• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • OSBC

Wajumbe wa Kamati ya Lishe Wilayani Kongwa Watakiwa Kuihamasisha Jamii Kutumia Lishe Bora

Imewekwa: July 12th, 2018

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt. Omary Nkullo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe amewaeleza wajumbe wa kamati hiyo kuwa lishe bora ni muhimu kwa Jamii, kwani lishe bora hupunguza Magonjwa ikiwemo Utapiamlo kwa Watoto.

Jamii inapaswa kutambua kwamba lishe bora ni muhimu kwa Watoto na inasaidia mtoto kuwa na Afya njema kimwili na kiakili, hivyo ni vema Jamii kutumia lishe bora kwa kuzingatia makundi ya vyakula, ikiwemo kundi la wanga, protini na vitamini. Aidha, amesisitiza kila mzazi kuhakikisha anachangia lishe mashuleni, kwani kwa kufanya hivyo wanafunzi wanaopata lishe bora hata uelewa wao pia utakuwa mzuri kuliko wasio na lishe bora.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Magreth Kagashe ambaye pia ni Katibu wa Kamati hiyo ya Lishe amesema, kwa sasa hali ya lishe Wilayani humo ni ya wastani, na kwa upande wa Tatizo la Utapiamlo kwa watoto hususani wa chini ya miaka mitano lipo.

Aidha, Dkt. Kagashe amesema, kumekuwa na Changamoto kubwa ya kutofautiana kwa Takwimu za Wilaya kuhusiana hali ya Utapiamlo na Taasisi Tofauti zinazofanya tafiti za Utapiamlo; Hali inayoleta Mkanganyiko kwa Jamii katika kutambua ukubwa wa Tatizo Wilayani humo.

Dkt. Kagashe amesema kuwa, kwa sasa Timu zilizoundwa kufanya Kazi ya kutambua ukubwa wa Tatizo hilo ikishirikisha wahudumu wa Afya 217 katika vijiji 87 vya Wilaya hiyo wapo katika hatua za mwisho kukamilisha zoezi hilo, hivyo Wilaya itatoa Takwimu halisi za Utapiamlo kwa mwaka 2017/2018 Ifikapo July 15.

Kufuatia mkanganyiko huo Wajumbe wa Baraza hilo wameazimia Taasisi zote zinazofanya Tafiti za lishe Ndani ya wilaya hiyo washirikishwe katika vikao vya Kamati hiyo ili nao waishirikishe Kamati vigezo wanavyotumia katika Tafiti wanazofanya ili kuondokana na mkanganyiko huo wa Takwimu za Hali ya Utapiamlo.

Pia, Dkt. Kagashe amesema Changamoto kubwa ya ukosefu wa lishe bora, ni Jamii kutokuwa na elimu ya Lishe bora, na kupelekea Jamii kushindwa kuhifadhi mazao hususani mazao ya  karanga, alizeti ambayo ni mazao muhimu katika lishe bora na kupelekea Jamii kutumia vyakula vya aina moja.

Kwa msisitizo amesema "Unakuta uji wa mtoto umechanganywa mahindi, mtama, mchele, uwele, ulezi ambazo ni nafaka tupu, wazazi wanakuwa wameuza karanga zote, kama ana ng'ombe maziwa yote anauza, mayai yote ya kuku yanauzwa, na kupelekea Mtoto anakuwa anakula chakula aina moja ambapo ni hatari kwa Afya".

Mwishowe,  Dkt. Kagashe amesisitiza kwamba Jamii iondokane na uuzaji wa vyakula vyote na badala yake iwe utamaduni wa kutunza mazao ya chakula ya aina mbalimbali kama karanga, nafaka, mazao aina za kunde ili kuwawezesha kujiepusha na Tatizo la Ukosefu wa Lishe Bora.

Sambamba na hayo Kamati imeshauri Muongozo wa Kamati ya Lishe ulioandikwa kwa Lugha ya Kiingereza utafsiriwe kwa Lugha ya Kiswahili kwani Lugha ya Kiingereza ni Changamoto kubwa katika Jamii ya kitanzania hasa ukizingatia muongozo huo utatumika kuanzia ngazi za Wilaya mpaka Vijiji.

Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2018. January 24, 2019
  • Tangazo la Nafasi ya Kazi January 16, 2019
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoa wa Dodoma Shule za Kutwa December 20, 2018
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoa wa Dodoma Shule za Bweni December 20, 2018
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • Wakulima Wahimizwa Kupambana na Viwavi

    January 31, 2019
  • Kongwa Yasaini Tamko la Kuhakikisha Kaya Zote Zinakuwa na Vyoo Bora Nakuvitumia

    December 07, 2018
  • Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Kuanza Wilayani Kongwa

    November 29, 2018
  • Benki ya NBC Yatoa Msaada wa Viti 80 na Kompyuta 15 kwa Halmashauri ya Kongwa

    November 14, 2018
  • Tazama Yote

Video

Usafi wa Mazingira ni Wajibu wa Kila Mtu.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)
  • Bunge la Tanzania

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Kongwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2320537

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. Haki zote zimehifadhiwa.