• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • OSBC

Wakulima na Wafanyabiashara wa Mazao Epukani Ufungashaji wa Lumbesa

Imewekwa: June 28th, 2018

Serikali kupitia Wakala wa Vipimo Tanzania Bara, inaendelea kuwasisitiza Wakulima na Wafanyabiashara wa mazao kuepuka ufungashaji wa lumbesa na kutumia vipimo halali kutokana na madhara Mengi yatokanayo na ufungashaji huo pamoja na kuhakikisha wanatumia mizani ambayo haijaharibika.

Afisa wa Wakala wa Vipimo Tanzania Bara, Mkoa wa Dodoma Bw. Saidi Ibrahim June 27, 2018 amewaeleza Wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Kongwa kuwa kazi kubwa inayofanywa na Taasisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania ni kusimamia matumizi sahihi ya Vipimo vya aina zote ili ikiwemo vipimo vya ujazo, uzito na urefu na kupiga marufuku Vipimo batili, yaani visivyo na ulinganifu.

Bw. Ibrahim amesema ufungashaji wa Lumbesa ni Ukiukwaji wa Taratibu za Vipimo na ameyataja madhara ya Lumbesa ni pamoja na kumpunja mkulima kutokana na ujazo huo kuzidi ujazo wa gunia la kawaida, hivyo mkulima hulazimika kuuza Lumbesa kwa bei ya ujazo wa kawaida.

Madhara mengine ni ya Kiafya kwa wabebaji, kutumia nguvu nyingi kupita uwezo wao na kutokuwa na uwiano kati ya Kilo za mbebaji na mizigo iliyofungashwa kwa mfumo huo wa Lumbesa, pia, huharibu miundombinu na kuharibu vyombo vya usafiri.

“Aidha, Lumbesa hudhoofisha ukusanyaji wa mapato, kwani mwenye mazao anapotozwa tozo kwa gunia moja huku amefungasha lumbesa ni dhahiri ufungashaji wa Lumbesa hupita vipimo halisia”. Amesisitiza Bw. Ibrahim.

Dinah Mlay ni mmoja wa Wafanyabiashara watumiao mizani ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Biashara kupitia Sekta Binafsi amesema, “kumekuwa na Changamoto za gharama kubwa za mafundi warekebisha mizani ambapo gharama hizo huzidi gharama ya manunuzi ya mzani mpya, hivyo anaomba Taasisi hiyo kuliangalia suala hilo kwa undani”. Aidha, Ibrahim alisema Faida ya Vipimo halisia vinakuza uchumi binafsi na uchumi wa Taifa, na kusaidia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi.

Ambapo Bw. Ibrahim amesema amelipokea na sehemu husika. Aidha,Sheria ya Vipimo inataka Vipimo vyote ikiwemo mizani, pampu za mafuta kukaguliwa na maafisa vipimo Mara moja kwa kila mwaka. Hivyo, Mlaji asipofanya hivyo, atakuwa amevunja sheria ya Vipimo

Pia, Bw. Ibrahim amesema Faida ya Vipimo halisia vinakuza uchumi binafsi na uchumi wa Taifa, na kusaidia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi.

Mwishowe, Wajumbe wa Baraza wakapata mafunzo ya Vitu muhimu vya kuzingatia katika Ufungashaji wa mvuto wa bidhaa mbalimbali, ambapo Bw. Ibrahim alibainisha kuwa ni kuhakikisha Bidhaa inakuwa na Jina, mahali inapotengenezwa, Jina la msambazaji, Anuani ya Posta, Barua pepe, Simu, Kiasi halisi cha Vipimo cha bidhaa, lugha inayotafsirika mahali inapoenda kuuzwa.


Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2018. January 24, 2019
  • Tangazo la Nafasi ya Kazi January 16, 2019
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoa wa Dodoma Shule za Kutwa December 20, 2018
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoa wa Dodoma Shule za Bweni December 20, 2018
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • Wakulima Wahimizwa Kupambana na Viwavi

    January 31, 2019
  • Kongwa Yasaini Tamko la Kuhakikisha Kaya Zote Zinakuwa na Vyoo Bora Nakuvitumia

    December 07, 2018
  • Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Kuanza Wilayani Kongwa

    November 29, 2018
  • Benki ya NBC Yatoa Msaada wa Viti 80 na Kompyuta 15 kwa Halmashauri ya Kongwa

    November 14, 2018
  • Tazama Yote

Video

Usafi wa Mazingira ni Wajibu wa Kila Mtu.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)
  • Bunge la Tanzania

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Kongwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2320537

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. Haki zote zimehifadhiwa.