• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
    • Miradi iliyokamilika
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • Michezo
    • Michezo
    • Sanaa

Mazingira na Usafi

1.0 MAJUKUMU YA IDARA:

1.1 HIFADHI YA MAZINGIRA

  1. Kutenga maeneo ya Upandaji Miti, Majani, Maua, ukataji Miti na Upendezeshaji Mazingira na kusimamia Kampeni ya Taifa ya upandaji Miti;
  2. Kuhamasisha Jamii kupanda Miti, Majani na Maua, ili kupendezesha Miji na maeneo mbalimbali;
  3. Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Halmashauri ya usimamizi wa Mazingira kwa kuzingatia Mpango kazi wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira;
  4. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo na miongozo ya kulinda Mazingira ikiwa ni pamoja na bioanui, Ardhi, Mazingira ya mito na mabwawa,
  5. Kubaini maeneo ya hatari yanayohitaji usimamizi maalumu na kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Usimamizi wa Mazingira kuhusu njia bora zinazoweza kutumika;
  6. Kuandaa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa;
  7. Kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji kwa Kudhibiti utekelezaji wa shughuli yoyote inayoweza kuleta athari katika maeneo ya mito na mabwawa.
  8. Kubaini Bioanui zilizopo katika Halmashauri na hali ya uharibifu na uhifadhi wake;
  9. Kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya Ardhi ya Halmashauri;
  10. Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na programu za Halmashauri kwa kuzingatia Mkakati wa matumizi Salama ya Teknolojia ya Kisasa (Biosafety);
  11. Kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala pamoja na majiko banifu;
  12. Kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali kuhusu Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira;
  13. Kutoa mapendekezo na kufuatilia hatua za kukabiliana na uharibifu wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (kama uchimbaji madini, kilimo, ujenzi, ufugaji n.k);

1.2 UDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA (ARDHI, MAJI NA SAUTI)

  1. Kuandaa na kutekeleza programu za kutoa elimu ya Mazingira kwa Jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa Mazingira na athari zake,
  2. Kuweka miongozo ya kupunguza athari za uchafuzi wa hewa ya ndani ya makazi (in-door pollution) inayosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile matumizi ya nishati ya kuni, vinyesi vya mifugo na uchomaji wa madini ya zebaki;
  3. Kufatilia na kutathimini athari za uchafuzi wa Mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo na ufugaji;
  4. Kuandaa na kusimamia miongozo ya kutenganisha maeneo ya makazi ya watu, ofisi na taasisi za elimu na shughuli za kiuchumi kama vile ujenzi wa viwanda, madampo ili kudhibiti athari kwa afya na Mazingira;

1.3TATHIMINI YA ATHARI YA MAZINGIRA

  1. Kufuatilia utekelezaji wa tathmini ya athari ya Mazingira [TAM] kwa shughuli zinazotakiwa kufanyiwa;
  2. Kufuatilia utekelezaji wa mpango na masharti ya TAM kwa kila shughuli/mradi uliofanyiwa tathmini hiyo au kukaguliwa;
  3. Kushirikisha umma katika maamuzi yanayoweza kuathiri Mazingira na katika uandaaji wa sera, mikakati, mipango na kufanya utafiti/uchunguzi wa uharibifu au athari ya Mazingira unaosababishwa na shughuli za kiuchumi au kijamii na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi mkuu NEMC
  4. Kufuatilia na kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizoendelevu kama vile uchimbaji madini holela, uvuvi haramu, kilimo kisichokuwa endelevu, ujenzi holela, ufugaji wa kuhamahama usiozingatia uwezo wa marisho n.k;
  5. Kusimamia/kuratibu utekelezaji wa kazi za kamati za Mazingira na kamati za kudumu za Halmashauri zinazoanzishwa na sheria ya usimamizi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri hadi kitongoji/mtaa;
  6. Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na program za Halmashauri kwa kuzingatia mkakati wa kitaifa wa kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi;

1.4 UDHIBITI TAKA NGUMU

  1. Kubuni mbinu za kupunguza taka na kusimamia utekelezaji wake ili kupunguza uchafuzi wa Mazingira;
  2. Kufanya tafiti/uchunguzi ili kubaini aina za taka zinazozalishwa kutoka katika masoko, makazi, maeneo ya barabara na taasisi pia kubuni njia bora za kupunguza, kutenganisha, kuhifadhi na kutupa taka;
  3. Kusimamia Usafi katika mifereji ya kukusanya maji ya mvua na kuhakikisha inafanya kazi muda wote;
  4. Kuweka vyombo vya kuhifadhi taka katika maeneo yote ya umma
  5. Kuainisha na kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa dampo za kisasa;
  6. Kutoa amri za kuzuia utupaji ovyo wa taka wa aina zote katika fukwe, maeneo ya wazi, mito na mifereji ya maji ya mvua;


2.0 CHANGAMOTO ZA KIMAZINGIRA:

  1. Uharibifu wa Misitu ya asili (Deforestation / Forest degradation)
  2. Uharibifu wa Mifumo ya ikologia ya Maji (River and Wetland Degradation),Mifumo na Vyanzo
  3. Uharibifu wa Ardhi (Land Degradation)
  4. Kupotea kwa Bionuai ( Loss of Biodiversity)
  5. Uharibifu na Uchafuzi wa Mazingira
  6. Mabadiliko Tabianchi (Climate Change)




..

Matangazo

  • Majina ya mipaka ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. October 16, 2024
  • TANGAZO LA MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 16, 2024
  • Tangazo la nafasi za ajira za mkataba October 07, 2024
  • Tangazo la kufunguliwa kwa dirisha la utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu- Oktoba 1 2024 October 02, 2024
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYASISITIZWA KUWA NA USHIRIKIANO MZURI NA VIONGOZI PAMOJA NA WATAALAM

    May 05, 2025
  • VIKUNDI 21 VYAKABIDHIWA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YA HALMASHAURI

    April 28, 2025
  • DC MAYEKA AKABIDHI MISAADA

    April 27, 2025
  • ZIARA YA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA MHE. WASIRA WILAYANI KONGWA.

    April 25, 2025
  • Tazama Yote

Video

zoezi la uandikishwaji daftari la Mpiga Kura kuanza 11-20 Oktoba, 2024
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Time huru ya Uchaguzi
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2370031

    Simu ya Mkononi: +255 713399349

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.