Sunday 23rd, February 2025
@Kongwa Mjini
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Dodoma itafanya Mkutano wake tarehe 25 – 27 Mei 2018.
Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na utaongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. White Zuberi Mwanzalila ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma.
Aidha, hii ni fursa nyingine kubwa na ya pekee kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kushiriki pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Dodoma kujadili masuala yenye manufaa kwa pande zote.
Mkutano huu unaambatana na ukaguzi wa miradi mitatu ya maendeleo ambayo ni; Ujenzi wa Kituo cha Afya Mlali; Ujenzi wa Machinjio ya Kuku Mbande; na Usambazaji wa Maji Kongwa Mjini.
Maandalizi ya Mkutano huu wa ALAT Mkoa wa Dodoma yamekamilika, wajumbe wote na waalikwa wanakaribishwa sana.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.