Tuesday 21st, January 2025
@Ukumbi wa Mikutano - Jengo la Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kongwa anawatangazia wananchi wote kuwa Zoezi la Uwekaji Wazi wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura litafanyika kwa siku nne tu; kuanzia tarehe 17 – 20 Juni, 2020.
Zoezi hili linahusisha kusahihisha taarifa za Wapiga Kura walioandikishwa awali, kuondoa waliokosa sifa, kuhamisha taarifa za Mpiga Kura na kutoa kadi mpya kwa waliopoteza kadi au kadi kuharibika.
Zoezi hili la Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litafanyika katika Kituo Kimoja tu kwa Wilaya nzima ambacho ni Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Elimu katika Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Kwa msaada kuhusu ufafanuzi wa zoezi hili la Uwekaji Wazi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wasiliana na Afisa Uchaguzi 0622750336.
Limetolewa na,
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kongwa
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.