Idara ya Afya ni miongoni mwa Idara 13 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Idara hii ina jumla ya vituo vya kutolea huduma vipatavyo 53 ambapo Hospitali ya Wilaya ni 1, Vituo vya Afya ni 5, na Zahanati 58, (Zahanati za Serikali 50, Mashirika ya dini5, binafsi 3).
Vile vile, Idara ya Afya inatoa huduma kwa jamii kama ifuatavyo:-
1. Huduma ya wagonjwa wa nje yaani (OPD),
2. Huduma ya kulaza wagonjwa yaani (Inpatient),
3. Huduma ya upasuaji mkubwa na mdogo,
4. Huduma ya mama na mtoto yaani (RCH),
5. Huduma ya CTC,
6. Huduma ya Kifua Kikuu na Ukoma,
7. Huduma ya wazee, huduma ya wagonjwa wa akili,
8. Huduma ya kinywa na meno, na
9. Huduma ya kuwasubirisha wamama wajawazito wenye vidokezo hatarishi (CHIGONELA).
Aidha, kuna Jengo la grade “A” kwa ajili ya kulaza wagonjwa wa makundi maalum, mfano bima ya afya na kadhalika.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.