Mwenye nia na uwezo wa kuanzisha Shule atume maombi ya kutaka kujenga shule kwa maandishi kwa Afisa Elimu
Kiongozi. Maombi haya yapitishwe kwa Afisa Elimu wa Wilaya Shule itakapojengwa na Afisa Elimu Mkoa yakiwa na viambatisho vifuatavyo:
Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na inahusisha yafuatayo:
Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na ya pili na inahusisha yafuatayo:
Usajili wa Shule za Kimataifa
Wizara husajili shule zenye hadhi ya kimataifa, usajili huo unafanywa na Taasisi za kimataifa zinazosajili Shule za aina hiyo. Wizara huthibitisha na kutambua shule zinazosajiliwa na taasisi hizo kama za kimataifa. Taasisi hizo ni “European Council for International Schools” (E.C.I.S) na “Association of International Schools in Africa (AISA). Taasisi hizo zimeweka vigezo vya
kusajili Shule za kimataifa. Shule itapewa usajili pale tu itakapotimiza vigezo vyote vilivyowekwa.
Hatua za kufuata ili Shule iwe ya Kimataifa
Mwenye Shule yeyote anayetaka Shule yake iwe na hadhi ya kimataifa anapaswa kufuata hatua zifuatazo:
Usajili wa shule/Taasisi za kidini
Taasisi za kidini zinazotaka kuanzisha na kuendesha Shule/Taasisi za kidini zinapaswa kufuata hatua zote tatu kama zilivyoelezwa isipokuwa wanapaswa kujaza fomu Na. RS.9 katika hatua ya usajili.
Tanbihi
Uvunjaji wa Sheria kwa namna yoyote ile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kifungu cha 59.
Ni nani anayehusika katika mchakato wa usajili wa shule?
Wakaguzi wa Shule; Maafisa Elimu; Wahandisi wa Majengo na Maafisa Afya wana wajibu mkubwa wa kuthibitisha kuwa maandalizi ya kutosha kuhusu majengo na mazingira ya Shule kiafya yanafaa kwa matumizi ya shule. Taarifa zinazoandaliwa na watendaji hao husaidia kutoa picha halisi ya matayarisho na kutoa mapendekezo sahihi pale wanapopitisha fomu za maombi ya kumiliki na kuendesha shule. Maombi haya huisaidia Wizara kupata picha halisi kuhusu matayarisho ya mwombaji na kufanya uamuzi sahihi.
Hutoa taarifa mahsusi zinazosaidia kutoa picha ya mahitaji ya Elimu katika eneo lao na kumthibitisha anayetaka kuanzisha Shule kama ndiye mmiliki halali wa eneo la Shule itakapojengwa.
Hufanya ukaguzi maalumu kwa lengo la kusajili shule na hukamilisha fomu Na RS. 8 kisha kutuma fomu hizo kwa Kamishina wa Elimu pamoja na taarifa ya Ukaguzi wa Shule husika. Mkaguzi Mkuu wa Shule husimamia na kutathimini utekelezaji wa mitaala pamoja na uendeshaji wa shule kwa ujumla.
Husimamia masuala yote ya maendeleo ya Elimu katika maeneo yao. Wanajukumu la kutoa maamuzi juu ya aina ya mipango inayotakiwa kufanywa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za serikali za msingi na za sekondari. Wanasimamia uhamasishaji wa maendeleo ya sekta ya elimu ya jamii inayowazunguka pia wanapokea na kupendekeza maombi ya kutaka kumiliki, kuendesha na kusajili Shule.
Waziri wa Elimu humthibitisha Mwenye Shule na huidhinisha usajili wa Shule za dini.
Usajili wa walimu unafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 sehemu ya VI na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 pamoja na Kanuni ya Elimu ya mwaka 2002.
Makundi matatu ya walimu yanayoweza kusajiliwa
Walimu wenye sifa
Walimu walio na taaluma ya ualimu ambao sio watanzania wanaotaka kufundisha nchini
Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982 unapatikana katika Ofisi za Elimu za Wilaya, Mkoa na Makao Makuu ya Wizara. Mwongozo huu unatoa tafsiri ya Sheria ya Elimu na Kanuni za Elimu kuhusu usajili wa shule na walimu.
Mambo muhimu yaliyopo katika mwongozo ni pamoja na fomu za usajili wa shule na walimu. Aina ya fomu (majina mapya katika mabano) hizo ni:
Fomu Mbalimbali:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.