Halmashauri hutoa huduma za upimaji wa viwanja na taratibu za utoaji wa hati, utatuzi wa migogoro ya mipaka, uuzaji wa viwanja vya serikali na upangaji wa miji kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili. Ili kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi, Halmashauri imeiongezea nguvu Idara ya Ardhi na Maliasili kwa kuongeza idadi ya watumishi wa kada hiyo wenye weledi, kuweka mipango thabiti ya kununua vifaa vya kisasa vinavyotumika katika shughuli za mipango miji na upimaji.
Aidha, mifumo ya TEHAMA inatumika katika kuharakisha utoaji wa huduma na taarifa kwa wananchi.