• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
    • Miradi iliyokamilika
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • Michezo
    • Michezo
    • Sanaa

DC Kongwa aagiza waliojifelisha darasa la saba kurudia

Imewekwa: January 8th, 2024

Na Stephen Jackson, Kongwa DC

Mkuu Mpya wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, ameagiza wanafunzi waliofeli mtihani wa darasa la Saba mwaka 2023 kinyume na matarajio kurudia darasa hilo ili kutimiza azma ya Serikali ya Kuifanya elimu ya kidato cha nne kuwa ya lazima.

Mhe. Mayeka alitoa agizo hilo Jumatatu Januari 08, 2024,  Katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mkoka wakati akizungumza na wazazi na walezi wa Wahitimu wa Darasa la saba mwaka 2023 waliofeli mitihani kinyume na matarajio yanayotokana na tathmini endelevu iliyofanywa na Divisheni ya elimu ya awali na msingi.

Katika hotuba yake alisema ni suala la aibu kupoteza muda kujadili suala la wazazi kuwa kikwazo kwa watoto wao kupata elimu katika ulimwengu wa Sasa na ameahidi kuihughulikia changamoto hiyo kikamilifu.

"Kwa muda ambao Mheshimiwa Rais ataniacha Kongwa, hili halitajitokeza". alisema Mayeka.

Hata hivyo ameipongeza Halmashauri kwa ya Wilaya ya Kongwa kwa kuweka utaratibu maalumu wa kuwasaidia wanafunzi wasio na uwezo kwa kuwalipia gharama za masomo katika ngazi mbalimbali za kielimu kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu.

Aidha Mhe. Mayeka Aliagiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kuhakikisha wanakwenda shuleni hata kama hawana sare za shule, na wazazi Kila mmoja ahakikishe anatoa ushirikiano wakutosha, ikiwa ni pamoja na kupeleka chakula kwani Kwa Imani yake anaamini kuwa Siri kubwa ya ufaulu wa mwanafunzi ni kupata chakula awapo shuleni. "Hakuna kitu chochote kinachosaidia ufaulu kwa wanafunzi zaidi ya wanafunzi kupata chakula Shuleni" alisema Mhe. Mayeka.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. White Zuberi Mwanzalilla amepongeza agizo hilo ambalo limetokana na maazimio ya vikao vya kisheria vya Halmashauri na kwamba uamuzi huo unalenga kuwakomboa wanafunzi hao na kwamba wasijihisi unyonge kwa kuwa dhamira ya uamuzi huo wa kuwarejesha shuleni ni kuwakomboa na siyo kuwaumiza.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji,  Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Mwalimu Margareth Temu alisema jumla ya Wanafunzi 416 wa darasa la saba walifeli mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka Jana (2023) kinyume na matarajio ingawa halmashauri ya  Kongwa inajivunia kupanda ufaulu kwa asilimia 8% ikilinganishwa na matokeo ya mwaka juzi.

Kati ya idadi hiyo wanafunzi wapatao 74, wanatokea tarafa ya Zoissa, ambapo 53 kati yao walishiriki kikao hicho muhimu.

Akizungumza kwa masikitiko, Spika mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Mhe. Job Yustino Ndugai alikemea tabia mbaya ya baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto wao kujifelisha kwa malengo ya kuajiriwa kazi za ndani na kuwataka kuacha mara Moja kwani kitendo hicho hakina faida yoyote.

Mhe. Ndugai aliwataka watoto hao kujitambua na kufahamu kwamba maisha yao ya baadaye yanategemea sana elimu yao hivyo wanao wajibu wa kushirikiana na wazazi wao kufanikisha ndoto zao, ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali ili kujikimu katika familia.

Mhe. Mayeka alisisitiza wazazi kuhakikisha watoto wao wanakwenda shuleni mapema iwezekanavyo yaani siku ya Jumanne ya tarehe 09 Januari, 2024 ili kuendelea na masomo ya darasa la saba, kwani hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayepuuza agizo hilo.

Sambamba na agizo hilo amewahimiza wazazi wote wenye wanafunzi shuleni kushirikiana na walimu kuboresha zoezi la ufundishaji na ujifunzaji kwa kuhakikisha wanafunzi hao wanapata chakula wawapo shuleni kwani inasaidia kuinua kiwango cha Ufaulu. " "Hakuna kitu chochote kinachosaidia ufaulu kwa wanafunzi zaidi ya wanafunzi kupata chakula Shuleni" alisema Mhe. Mayeka.

Ili kukomesha tabia ya watoto kuajiriwa kazi za ndani katika miji mbalimbali, alitoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kuwafichua madalali wote  wanaojihusisha na kushawishi watoto wenye umri wa kuwa shuleni kwenda kufanya kazi za ndani.

Katika kikao hicho Wataalamu ngazi ya Wilaya, kata na vijiji wakiwemo Walimu, walichangia mawazo yao, kubwa zaidi wakiahidi kushirikiana na wazazi katika jitihada za  kuondoa changamoto hiyo ya aibu ya kujifelisha kwa wanafunzi.

Kufuatia hali hiyo, Mhe. Mayeka amewaagiza watendaji wa Kata zote kuwasaka wanafunzi wote waliojifelisha watafutwe popote walipo ili waweze kurejea shuleni na kuendelea na  masomo ya darasa la saba.


Matangazo

  • Majina ya mipaka ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. October 16, 2024
  • TANGAZO LA MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 16, 2024
  • Tangazo la nafasi za ajira za mkataba October 07, 2024
  • Tangazo la kufunguliwa kwa dirisha la utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu- Oktoba 1 2024 October 02, 2024
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • MGOGORO WA MPAKA CHIGWINGWILI - HOGORO KUTAFUTIWA UFUMBUZI.

    May 08, 2025
  • VIKUNDI VYASISITIZWA KUWA NA USHIRIKIANO MZURI NA VIONGOZI PAMOJA NA WATAALAM

    May 05, 2025
  • VIKUNDI 21 VYAKABIDHIWA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YA HALMASHAURI

    April 28, 2025
  • DC MAYEKA AKABIDHI MISAADA

    April 27, 2025
  • Tazama Yote

Video

zoezi la uandikishwaji daftari la Mpiga Kura kuanza 11-20 Oktoba, 2024
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Time huru ya Uchaguzi
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2370031

    Simu ya Mkononi: +255 713399349

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.