DC KONGWA AKAGUA UCHIMBAJI WA MADINI NDURUGUMI
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka ametembelea na kukagua uchimbaji wa madini unaofanyika katika Mamlaka ya Mji mdogo Kibaigwa eneo la Ndurugumi Wilayani Kongwa na kuongea na Wachimbaji wa Madini katika eneo hilo.
Mhe. Mayeka akiwa ameambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama, wataalam wa Halmashauri na viongozi wa Kata ya Kibaigwa amefanya ukaguzi huo mwishoni wa juma lililopita ili kijiridhisha na hali ya usalama na usafi wa mazingira wa maeneo hayo.
Katika mkutano huo Mhe. Mayeka ameeleza kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea maeneo ya uchimbaji madini kufungwa kama kutokuwepo kwa vyoo bora, utoroshaji wa madini, utumikishwaji wa watoto chini ya miaka 18 na akina mama wajawazito.
Vilevile Mhe. Mayeka ameagiza ofisi ya mazingira kuhakikisha usafi wa mazingira wa maeneo hayo pamoja na ujenzi wa vyoo bora kuelekea msimu wa mvua ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Aidha Mhe. Mayeka amehimiza wachimbaji kuepuka uchimbaji holela kwani ni hatari hivyo kuwe na utaratibu mzuri ambao utawasaidia kulinda afya zao na mazingira kwa ujumla.
Kwa upande wao wachimbaji hao wameomba Serikali kuweka utaratibu mzuri wa bei ya madini suala ambalo Mhe. Mayeka amewataka wenye leseni kuweka utara
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.