MAYEKA AFANYA KIKAO CHA NDANI NA VIONGOZI WA KIJIJI CHA CHIGWINGWILI
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka amezitaka kamati ya wafugaji na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Chigwingwili kuacha migongano inayorudisha nyuma maendeleo ya Kijiji hicho badala yake kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe. Mayeka akiwa ameambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya ameeleza hayo katika kikao cha ndani na viongozi wa Kijiji cha Chigwingwili kilichopo Kata ya Mtanana Wilayani kongwa alipofika kwa ajili ya kutatua changamoto za migogoro baina ya kamati ya wafugaji na wajumnbe wa serikali ya Kijiji.
Katika hatua hiyo Mhe. Mayeka amesema ataendelea kufuatilia na kuchunguza chanzo cha migogoro Kijijini hapo na kuitaka kamati ya wafugaji kutambua kuwa haiko juu ya Halmashauri ya Kijiji na wala Kijiji sio mali ya mwenyekiti.
Akiongea katika kikao hicho mhe. Mayeka amemtaka mwenyekiti wa Kijiji hicho ndg. Petro Matambo kuangalia namna nzuri ya kuwasimamia wafugaji bila kuleta migogoro na kuhakikisha fedha zote zinawekwa kwenye akaunti ya Kijiji na kutolewa kwa mhutasari.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.