• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kongwa District Council
Kongwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Idara ya Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi & Zima moto
      • Mazingira na Usafi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Madini
    • Biashara
    • Viwanda
    • Mawasiliano
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Ardhi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za TEHAMA
    • Usimamizi & Ufuatiliaji wa Miradi
    • Huduma za Ushauri na Ufundi
    • Ruzuku ya Kunusuru Kaya Masikini
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Inayoendela
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
    • Miradi iliyokamilika
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala
      • Maendeleo ya Jamii
      • Nishati
  • Machapisho
    • Sheria ndogo ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida
    • Gazeti la Serikali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video za Shughuli za Maendeleo
  • Michezo
    • Michezo
    • Sanaa

Ndugai awataka wananchi kuchangamkia fursa za Mafunzo VETA

Imewekwa: May 14th, 2023

Na Stephen Jackson, KDC

Mbunge wa Jimbo la Kongwa Mhe. Job Yustino Ndugai amewataka wananchi kuchangamkia fursa za Mafunzo yanayotolewa na chuo cha Ufundi Stadi VETA - Kongwa Ili kujipatia ujuzi mbalimbali utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Ndugai amesema hayo muda mfupi baada ya ibada ya Jumapili iliyofanyika katika kanisa la Anglikana la chuo cha Theolojia cha Mt. Philip's  Mjini Kongwa ambapo alialikwa kama mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa Maendeleo ya Kanisa na Jamii, (Church and Community Mobilization Project - CCMP) unaotekelezwa katika vijiji (10) katika ukanda wa Hogoro na Zoissa.

Mradi huo unajihusisha na utoaji wa Elimu juu ya matumizi sahihi ya maji kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi, na kusimamiwa na Mchungaji Canon Agripa Ndatila kama mshauri Mkuu.

Akizungumzia chuo hicho Mhe. Ndugai amesema Mafunzo yanayotolewa na VETA ni muhimu na gharama yake ni nafuu ambayo kila mwananchi anaweza kuyamudu.

Ikiwa ni Sehemu ya kuadhimisha siku ya familia  duniani, Katibu wa umoja wa akinamama wa kanisa la Anglikana Tanzania (UMAKI) Bi. Margareth Ndonde aliyehubiri katika ibada hiyo amewataka akinamama kutoka kwenye familia za wachungaji, kujihusisha na shughuliza kiuchumi ili kuepuka kuwa tegemezi. Aliongeza kuwa familia zenye ustawi bora ni zile yenye  kushirishana mambo mbalimbali na kutunza siri.

Katika mwendelezo wa ujumbe wake, Bi. Ndonde alisisitiza familia kujenga mahusiano mema na majirani ili kuimarisha amani katika jamii.

Kwa mujibu wa Bi. Margareth Ndonde, Umoja huo kwa mara ya kwanza utajenga shule ya Sekondari yenye Kidato cha Kwanza hadi cha Sita mkoani Dodoma kupitia michango yao.

Naye Mchungaji wa Kanisa hilo  Canon Agripa Ndatila alimpongeza Mhe. Ndugai kwa kauli yake ambayo amekuwa Akiitoa Sehemu mbalimbali kuwa ifikapo Mwaka 2025 ataachia kwa hiari nafasi hiyo ili kutoa fursa kwa wengine kuongoza.

Katika hafla hiyo, Mhe. Ndugai alikata utepe na kutia Saini katika bango maalumu la mradi kama ishara ya uzinduzi, kisha kukabidhi pikipiki mbili (2) aina ya Boxer  kwa matumizi ya mradi ambapo awali alikabidhi vyeti kwa wanachama wapya wa Umoja wa akinamama wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa Risala iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi, chuo cha Mt. Philip's kinakabiliwa na changamoto ya barabara tangu kilipoazishwa Mwaka 1914 , jambo ambalo Mhe. Ndugai aneahidi kulishughulikia katika kipindi cha miaka miwili.

Matangazo

  • Majina ya mipaka ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. October 16, 2024
  • TANGAZO LA MAELEKEZO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024. October 16, 2024
  • Tangazo la nafasi za ajira za mkataba October 07, 2024
  • Tangazo la kufunguliwa kwa dirisha la utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu- Oktoba 1 2024 October 02, 2024
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • MGOGORO WA MPAKA CHIGWINGWILI - HOGORO KUTAFUTIWA UFUMBUZI.

    May 08, 2025
  • VIKUNDI VYASISITIZWA KUWA NA USHIRIKIANO MZURI NA VIONGOZI PAMOJA NA WATAALAM

    May 05, 2025
  • VIKUNDI 21 VYAKABIDHIWA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YA HALMASHAURI

    April 28, 2025
  • DC MAYEKA AKABIDHI MISAADA

    April 27, 2025
  • Tazama Yote

Video

zoezi la uandikishwaji daftari la Mpiga Kura kuanza 11-20 Oktoba, 2024
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalmbali
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Miongozo
  • Miradi iliyokamilika
  • Miradi inayoendelea
  • Taarifa kwa Umma
  • Zabuni
  • Kituo cha Biashara (OSBC) Kongwa
  • Orodha ya Madiwani na Mawasiliano

Viunganishi Linganifu

  • Time huru ya Uchaguzi
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA)

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Rekodi ya Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya

    Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma

    Simu ya Mezani: +255 26 2370031

    Simu ya Mkononi: +255 713399349

    Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti
    • Tahadhari kwenye Barua pepe

Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.