Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amewataka wasimamizi wa miradi mbalimbali ya kijamii inayotumia fedha za umma kuandaa bajeti zenye tija Ili kuyafikia malengo ya miradi hiyo badala ya kuweka vipaumbele kwenye malipo ya posho na maslahi binafsi.
Mhe. Mwema amesema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) kilichofanyika Oktoba 13, 2023 katika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
Akiwasilisha mada katika kikao hicho kuhusu mradi wa Uendelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira "P4R" Afisa Afya Wilaya bwana Abdulrahman Shehe Othman ametaja malengo ya mradi huo kuwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya Maji na Usafi wa Mazingira katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya katika Halmashauri, Kuhamasisha ujenzi na matumizi ya vyoo bora katika ngazi ya kaya pamoja na kuhimiza tabia ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
Programu ya "P4R" inatekelezwa Kwa ushirikiano wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania kupitia "force Account" katika Halmashauri 137 ndani ya mikoa 25 ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024, Mkoa wa Dodoma na Halmashauri 6 zikiwa ni miongoni mwa wanufaika katika awamu ya pili ambapo jumla ya Shilingi 238,848,519.12 zimepokelewa katika maeneo ya utekelezaji Wilayani Kongwa.
Programu hiyo inatekelezwa katika zahanati tatu za Manyata, Hembahemba na Msunjilile ambazo zimetengewa jumla ya shilingi 160,723,614.00 huku CHMT ikitengewa Shilingi 78,124,905.12
Wa pili kulia ni Afisa Afya (W) Abdulrahman Shehe Othman akisikipokea michango ya mawazo mara baada ya kuwasilisha mada. Picha na Stephen Jackson.
Naye Mratibu wa Chanjo na mnyororo baridi Kongwa (DIVO) Bwana Cosmas Mlimila aliwasilisha mada kuhusu Tahadhari ya Mlipuko wa ugonjwa wa Surua, na kwamba huduma ya chanjo kwa watoto wote ambao hawakukamilisha au kutochanja kabisa inatarajiwa kutolewa Kwa misingi ya dharula.
Mlimila amezitaja dalili za ugonjwa wa Surua kuwa ni pamoja na Homa kali, Vipele, Macho kuwa mekundu, Kikohozi na Mafua Huku athari zake zikiwa ni Nimonia kali Upofu wa Macho, Homa ya uti wa mgongo na hatimaye Kifo. Aidha alifafanya kuwa ugonjwa wa Surua husambazwa kwa njia ya Kikohozi au chafya kutoka kwa mtu aliyeambukizwa na dalili zake huweza kuonekana kuanzia siku 7 hadi 18.
Miongoni mwa Mikakati ya kukabiliana na Ugonjwa wa Surua Wilayani Kongwa ni pamoja na kuwatafuta watoto wote ambao hawajakamilisha chanjo au kutochanja kabisa, utoaji wa Elimu Kwa Jamii na kuhakikisha upatikanaji wa chanjo na kuimarisha huduma za mkoba.
Katikati ni Bwana Cosmas Mlimila, Mratibu wa Chanjo na mnyororo baridi (DIVO) akifuatilia mjadala baada ya kuwasilisha mada ya tahadhari ya mlipuko wa Surua.
Mhe. mwema alihitimisha kikao hicho kwa kusisitiza mapitio ya bajeti katika mradi wa "P4R" Ili kuhakikisha tija inakuwepo Kwa kuleta Matokeo chanya huku Suala la tahadhari ya mlipuko wa Surua likisimamiwa kikamilifu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.