SERIKALI YATOA MWONGOZO KWA WATUMISHI WANAOJITOLEA
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari Kongwa DC
Idara ya utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imekutana na watumishi wanaojitolea katika Idara na vitengo mbalimbali ili kuwasomea na kuwafafanulia mwongozo wa kujitolea katika Utumishi wa Umma uliotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Akiongea katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 20 Januari 2026 Mkuu wa Idara ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Ndg. Fortunatus Mabula amesema kuwa ufafanuzi wa mwongozo huo ni utekelezaji wa maagizo ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unaoeleza kwa kina namna Taasisi za Umma zinavyotakiwa kupata Watumishi wa kujitolea kufanya kazi kwa masharti yasiyo ya kudumu.
Nae Ndg. Benson Nduhila Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa amefafanua kwa kina sifa na malengo mahususi ya Mwongozo huo ikiwemo kuweka utaratibu wa kuwapata, kuwapanga na kuwatumia vijana wanaojitolea.
Aidha Ndg. Nduhila ameongeza kuwa mwongozo unawataka waajiri kuwapa kipaumbele vijana wote wakiwemo walemavu, kufanya mahojiano ya kina kuhakikisha kila mwombaji anakuwa na nafasi ya kuhojiwa na hatimaye kuchaguliwa kwa haki na usawa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.