TIMU YA UFATILIAJI NA TATHMINI WILAYANI KONGWA YATEMBELEA MIRADI YA UJENZI
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari – Kongwa DC
Timu ya ufuatiliaji na tathmini Wilayani Kongwa imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ya Elimu na Afya.
Katika kukagua miradi hiyo timu imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi unaoendelea ambapo mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini Bi. Christina Chihimba amewataka mafundi kuharakisha ujenzi ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa na wananchi waweze kunufaika na miundombinu hiyo.
Baadhi ya miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa madarasa 5 na matundu 12 ya vyoo yenye thamani ya Tsh milioni 143,800,000 inayojengwa kwa fedha za BOOST katika shule ya msingi Mgoloka iliyopo Kata Chitego na mradi wa madarasa 4 ofisi 2 za walimu na matundu 6 ya vyoo vyenye thamani ya Tsh milioni 103,200,000 fedha za BOOST katika shule ya Msingi Mnuku iliyoko Kata ya chitego.
Miradi mingine ni madarasa 5 na matundu 12 ya vyoo elimu msingi vyenye thamani ya Tsh milioni 136,400,000 fedha za BOOST katika shule ya msingi Tubugwe Kibaoni Kata ya Chamkoroma na mradi wa madarasa 2 ya awali matundu 6 ya vyoo vyenye thamani ya Tsh milioni 64,600,000 fedha za BOOST katika sule ya msingi mbagilwa iliyoko Kata ya Ng’humbi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.