Idara ya Utumishi Na Utawala inatoa huduma mbalimbali kama ifuatavyo:
Kuajiri (Kuingiza watumishi wapya kwenye payroll
Kupandisha vyeo watumishi wa idara mbalimali (Promotion.)
Kuwaondoa kwenye payroll watumishi waliostaafu, kufariki, kuacha kazi na utoro wa muda mrefu.
Usimamizi wa watumishi katika maslahi mbalimbali ya kiututumishi kama nidhamu.
Kusimamia taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System (HCMIS-Lawson).
Kuandaa mpango wa mafunzo wa halmashauri na mahitaji ya mafunzo kwa watumishi.
Kuratibu mahudhurio ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Kuandaa taarifa za idara, taarifa za Tume ya Utumishi wa Umma, taarifa za utekelezaji za robo mwaka.
Kutunza na kujaza rejesta za taarifa mbalimbali za watumishi mfano walioacha kazi, watoro, waliofariki, waliohama, waliohamia, waliostaafu.
Kuratibu mpango wa likizo ya mwaka kwa watumishi “Leave roster.
Kusimamia suala la ujazaji wa fomu za OPRAS kwa watumishi wa Halmashauri na Idara ya Utawala.
Kuandaa takwimu za kiutumishi za Halmashuari.
Kuandaa na kusimamia sera ya usimamizi na uendeshaji wa ofisi ya Halmashauri.
Kuandaa bajeti ya idara ya utawala kwa kila mwaka wa fedha.
Kuandaa mpango wa manunuzi wa Idara ya Utawala.
Kusimamia watendaji wa vijiji na kata kuhusu kuitisha mikutano ya kisheria na utekelezaji wa shughuli za utawala bora.
Kuandaa taarifa ya kila robo ya mikutano ya kisheria iliyofanyika kwa ngazi zote na kuiwasilisha katika taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Serikali za kila robo.
Kuandaa bajeti ya mishahara (PE) na kuingiza kwenye mfumo wa taarifa za kitumishi na mishahara.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.