Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kongwa, CPA Deodatus Mutalemwa amemtangaza ndg. Mngurumi Isaya Moses wa Chama cha Mapinduzi kuwa mshindi wa kiti cha ubunge jimbo la Kongwa kwa kura 217,416 akiwashinda ndg. Rejina Sembuche wa AFP ambaye amepata kura 3,269, Ndg. Mayewu. M. Jerald ambaye amepata kura 3,521 na ndg. Sunday J. Madinda ambaye amepata kura 5,261. Akiongea baada ya kutangazwa mshindi na kupokea hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kongwa, ndg. Mngurumi ameshukuru chama chake kwa kumpatia ridhaa ya kugombea nafasi hiyo na kushukuru Tume ya uchaguzi kwa ufanisi pamoja na uwazi walioonyesha katika zoezi zima la uchaguzi, pia ndugu Mngurumi ameshukuru vyama pinzani ambavyo vimeweka ushindani katika zoezi la uchaguzi. shukrani zake nyingine zimeenda kwa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vimefanya kazi kubwa kuhakikisaha ulinzi na usalama

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.