Kitengo cha Uchaguzi ni miongoni mwa vitengo 6 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa vilivyoanzishwa kwa mujibu wa Muundo wa Halmashauri wa mwaka 2012.
Kitengo hiki kilianzishwa mahususi kwa ajli ya kusimamia na kuratibu shughuli zote za uchaguzi Mkuu na Chaguzi ndogo za Urais, ubunge na Udiwani kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Kanuni za Uchaguzi na Maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ngazi ya Halmashauri.
Pia kitengo hiki kinawajibika kusimamia na kuratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu na Chaguzi ndogo za Serikali za Mitaa kwa Mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi na Maelekezo ya Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Dira ya Kitengo hiki ni Kuwa kitengo madhubuti kitakacho weza kuchangia katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa kujenga Halmashauri inayozingatia Utawala bora uliojengwa katika misingi ya Uchaguzi Huru, wa Haki na wa Mara kwa mara (Free, Fair and Frequent elections) kufikia 2025 .
Dhima ya kitengo hiki ni kuhakikisha kuwa Sheria na Kanuni za Uchaguzi zinasimamiwa ipasavyo kwa lengo la kuwawezesha Wananchi wote wenye sifa katika Halmashauri kupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika kuwachagua viongozi wao kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki.
Toka kuanzishwa kwake kitengo hiki kimeweza kupata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Uchaguzi. Mafanikio hayo ni Pamoja na:
Kusimamia kwa ufanisi Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.