Halmashauriya Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa wilaya saba (7) za mkoa wa Dodoma, ilianzishwa mwaka1996 chini ya sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 kifungu Na. 8 naNa. 9. Wilaya ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 4,041 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo naufugaji ni hekta 363,690.Wilaya ina Tarafa 3 za Kongwa, Mlali na Zoissa, Kata 22, Vijiji 87,Vitongoji 383 naMamlaka za miji midogo miwili ya Kongwa na Kibaigwa. Wilaya imepakana na Wilayaya Chamwino upande wa Magharibi; Wilaya ya Gairo (Mkoa wa Morogoro), upande waMashariki; Wilaya ya Mpwapwa upande wa Kusini na kwa upande wa Kaskazini kuna Wilaya ya Kiteto (Mkoa wa Manyara).
Kwa mujibu wasensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Wilayaina ongezeko la watu laasilimia 2.4; Hivyokwa mwaka 2015 wilayaya Kongwa inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 332,831 ambapowanaume ni 160,225 na wanawake ni 172,606. Aidha,Idadi ya kaya zilizopo kwa sasa ni 61,994. Kaya zinazojihusisha na shughuli za kilimo pamoja na ufugaji ni 55,573 sawa na 90%.
Wenyeji wa Wilaya hii ni Wagogo, Wakaguru, na Warangi. Pia kuna makabila mengine ambayo yalihamia toka sehemu mbambali za Tanzania kama vile Wabena, Wanguu, Wakamba na Wamasai ambao walikuja kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo.
Shughuli kuu za kiuchumu zinazofanywa na wakazi wa Wilaya ya Kongwa ni ufugaji wanyama (ng’ombe, mbuzi, kondoo, na punda). Punda hutumika zaidi katika usafirishaji wa mazao. Pia shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na biashara mfano mahindi, mtama, uwele, karanga na alizeti.
Wilaya ya Kongwa lianza kujulikana katika ramani ya Dunia mwaka 1913 ambapo Shirika la Kidini kutoka Canada ambalo lilijulikana kama Church Missionary Society walipoanza ujenzi wa Chuo cha Ualimu na Theolojia mwaka 1909 katika kijiji cha Mlanga. Lakini kutokana na Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, ujenzi huo ulichukua muda mrefu hivyo kukamilika mwaka 1927. Vifaa vilivyotumika katika kujengea Chuo hicho ni mawe na chokaa iliyochomwa.
Chuo kilifundisha taaluma ya Uchungaji (Theolojia), Ualimu na Uuguzi. Wanafunzi waliosoma katika Chuo hicho walitoka sehemu mbalimbali za Tanganyika na Kenya. Miongoni mwa wanafunzi wa kwanza waliosoma katika Chuo hicho ni Mzee Musa Fungo na Yohana Malecela.
Jengo la Chuo cha Theolojia cha Mtakatifu Filipo kilichojengwa mwaka 1927 – Mlanga Kongwa
Wakati wa vita ya Wakoloni baina ya Waingereza na Wajerumani mwaka 1914 – 1918, wanafunzi 12 walisoma katika Chuo hicho walikamatwa na Wajerumani na kupelekwa Zanzibar kuhifadhiwa na vita ilipoisha walirudishwa. Wakazi wengi walioishi katika eneo la Mlanga, wengi wao ni wahamiaji toka sehemu za Berege (Morogoro), Tanga na Iringa na Kiongozi wao kwa kipindi hicho alikuwa anaitwa Chifu Mahinyila. Katika eneo la Mlanga karibu na mlima kuna alama za miguu ya Farasi ambao walipitishwa katika njia hiyo na Wakoloni wakati wa vita.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.