1. Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya.
Mradi huu unajumuisha ujenzi wa Jengo la utawala, wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la Uzazi(Maternity, na jengo la Kuhifadhia Maiti (Mortuary). Mradi huu unagharimu shilinngi Bilioni Moja (1000,000,000) zilizotolewa na Serikali kuu.
2. Ujenzi wa kituo cha Afya Songambele
Mradi huu unatekekelezwa kwa fedha za Serikali kuu Tzs 400,000,000 na upo katika hatua za mwanzo.
3. Ujenzi wa kituo cha afya Kibaigwa
Ujenzi wa Kituo hiki unagharimu TZS Milioni mia tano (5000,000,000/=) Ambazo zimetolewa na Ubalozi wa Japan.
4. Ujenzi wa kituo kipya cha afya kata ya Chamkoroma
Mradi huu unajumuisha Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la upasuaji (Theatre), jengo la uzazi (Maternity) na Jengo la Maabara(Laboratory)
5. Ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Pandambili
Mradi huu unagharimu Milioni Thelathini (30,000,000/=) ambazo zimetolewa na Serikali Kuu
6. Ukamilishaji wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Manghweta
Mradi huu unagharimu TZS Milioni Mia Ishirini na tano (25,000,000/=) Ambazo zimetolewa na Serikali kuu.
7. Ukamilishaji wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Tubugwe Juu
Ujenzi wa mradi huu unagharimu TZS Milioni Mia Ishirini na tano (25,000,000/=) Ambazo zimetolewa na Serikali kuu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.