Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ni miongoni mwa Idara 13 za Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa. Idara inajishughulisha na shughuli za mifugo na uvuvi ikiwa ni pamoja na kutoa tiba, chanjo, ukaguzi wa nyama katika machinjio na makaro na kutoa ushauri wa kitalamu kwa wafugaji.
Idara ina jumla ya Watumishi 28 wa fani mbalimbali kama inavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo:
NA
|
KIWANGO CHA ELIMU
|
IDADI
|
1.
|
Shahada ya Uzamili
|
4
|
2.
|
Shahada ya Kwanza
|
5
|
3.
|
Stashahada
|
14
|
4.
|
Astashahada
|
5
|
|
JUMLA
|
28
|
Maeneo ya malisho ya mifugo ni hekta 105,000 likiwepo eneo la ranchi ya Taifa ya Mifugo (NARCO) – Kongwa lenye ukubwa wa Ha. 37,682 na Kituo cha utafiti wa malisho ya mifugo (PRC) chenye ukubwa wa Ha. 2,243.
Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO ina shamba la mifugo katika Wilaya ya Kongwa. Shamba hilo lina ukubwa wa hekta 37,682 zenye uwezo wa kufuga kwa wakati mmoja ng’ombe 14,000. Mifugo ifugwayo katika shamba hilo ni pamoja na ng’ombe aina ya Borani, Mbuzi na Kondoo aina ya Black Headed Persian. Shamba hili lilianzishwa mnamo mwaka 1947 kipindi ambacho mashamba ya Karanga yalianzishwa na kampuni ya Overseas Food Corporations ili kutoa huduma ya kutoa nyama katika mashamba ya Karanga.
Kituo cha utafiti wa malisho ya mifugo kipo upande wa kaskazini mashariki mwa kijiji cha Mbande. Kituo hiki hujishughulisha zaidi na utafiti wa malisho kwa ajili ya mifugo lakini pia hufanya tafiti za koosafu bora za mifugo. Kituo kina eneo la ukubwa wa hekta 2,243, Kituo hiki kinafuga wanyama kama vile Mbuzi aina ya Blended na Ng’ombe chotara wa maziwa.
Mifugo huchukua nafasi ya pili kiuchumi baada ya kilimo. Ufugaji pia ni sehemu ya jadi ya wakazi wengi wa Wilaya ya Kongwa ambayo ina hazina kubwa ya aina mbalimbali ya mifugo kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo:-
Aina ya Mifugo
|
Idadi ya Mifugo |
||||
Mifugo Bora |
Kienyeji
|
Jumla
|
|||
Maziwa
|
Nyama
|
Mayai
|
|||
Ng’ombe
|
280 |
6,799 |
|
117,438 |
124,517 |
Mbuzi
|
506 |
52 |
|
79,235 |
79,793 |
Kondoo
|
|
685 |
|
35,977 |
36,662 |
Nguruwe
|
|
|
|
35,932 |
35,932 |
Punda
|
|
|
|
2,709 |
2,709 |
Kuku
|
|
|
10,362 |
446,054 |
456,416 |
Bata
|
|
|
|
6,382 |
6,382 |
Kanga
|
|
|
|
962 |
962 |
Mbwa
|
|
|
|
1,073 |
1,073 |
Sungura
|
|
130 |
|
120 |
250 |
Farasi
|
|
|
|
|
7 |
(Kwa mwaka 2012/2013)
Kiwango cha ongezeko la baadhi ya mifugo hii kwa mwaka ni kama ifuatavyo:-
Ng’ombe 2.9%
Mbuzi 4%
Kondoo 4%
Nguruwe 5%
Miundo mbinu ya mifugo iliyopo ni kama ifuatavyo:-
Na
|
Aina ya miundo mbinu
|
Mahitaji |
Iliyopo |
Pungufu |
Inayofanya kazi |
Isiyofanya kazi |
1
|
Majosho
|
25 |
21 |
4 |
16 |
5 |
2
|
Vituo vya Maendeleo ya Mifugo
|
14 |
4 |
10 |
2 |
2 |
3
|
Mabirika ya maji
|
59 |
19 |
40 |
16 |
3 |
4
|
Vibanio
|
52 |
4 |
48 |
3 |
1 |
5
|
Malambo
|
44 |
14 |
30 |
8 |
6 |
6
|
Minada
|
11 |
9 |
2 |
4 |
5 |
7
|
Vituo vya ukaguzi wa mifugo
|
3 |
3 |
0 |
1 |
2 |
8
|
Machinjio ndogo
|
7 |
5 |
2 |
4 |
1 |
9
|
Makaro ya kuchinjia
|
14 |
9 |
5 |
9 |
0 |
10
|
Mabanda ya ngozi
|
18 |
6 |
12 |
4 |
2 |
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.