DC KONGWA ASISITIZA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari – Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka amewakumbusha wananchi hususani vijana kutimiza suala la kikatiba la uchaguzi kwa kupiga kura kwani ni haki yao ya msingi kwa maendeleo ya taifa zima la Tanzania.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Pandambili wakiwa katika mkutano.
Mhe. Mayeka ameyasema hayo alipokuwa katika ziara zake za kawaida za kikazi alipotembelea na kuongea na wananchi wa Kata za Pandambili na Mtanana ambapo amewataka vijana kuwa na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na si kupotoshana juu ya masula ya msingi kama uchaguzi.
Aidha Mhe. Mayeka amewasisitiza Wananchi kudumisha amani na utulivu kipindi cha uchaguzi mkuu na kuwaomba wazazi kuongea na vijana wao juu ya kujua umuhimu wa amani tuliyonayo na madhara ya kuipoteza amani.
Katika hatua nyingine Mayeka ametumia hadhara hiyo kuzitaka taasisi za umma kama Shule na vituo vya Afya kulipa bili za maji kwa wakati ili kurahisisha utoaji wa huduma hiyo.
Baadhi ya wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wakiwa katika mkutano wa hadhara.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.