UTANGULIZI:
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ni Sekta mtambuka na ni miongoni mwa idara kumi na tatu (13) zinazounda Halmashauri ya wilaya ya Kongwa. Idara inatekeleza majukumu yake kulingana na Miongozo na Sera mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa kuzingatia dira na mwelekeo wa kitaifa na dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa..
HALI YA HEWA:
Zaidi ya asilimia 90 ya eneo la Wilaya la hekta 404,100 linafaa kwa kilimo na Ufugaji, shughuli ambazo ni msingi mkubvwa wa uchumi wa wakazi wa Wilaya hii.kwa sasa eneo linalotumika kwa kilimo na Mifugo linakadiriwa kufikia hekta 363 , 690 na lisilofaa halitumiki ni hekta 40,410.
Aidha eneo linalofaa kwa kilimo linakadiriwa kuwa hekta 323,590. Eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji Maji mashambani ni hekta 5,811 na kiwango kinachotumika ni hekta 422kwa njia ya asili. Hali ya upatikanaji wa mvua ni kati ya mm 400-800 kwa mwaka.
Aidha kulingana na kiwango cha upatikanaji wa Mvua, Wilaya imegawanywa katika kanda mbili za uzalishaji wa Mazao ya Kilimo ambazo maeneo yannayopata Mvua zaidi ya mm 600kwa mwaka na uUkanda wa pili ni maeneo yanayopata mvua kati ya mm 400 hadi 6600 kwa mwaka. Kipindi cha Mvua ni kifupi ambacho huanza mwezi Novemba hadi Aprili kwa kanda inayopata mvua chini ya mm 600na mei kwa ukanda wenye mvua nyingi. Maeneo yalioko katika ukanda unaopata mvua chini ya mm 600 ni vijiji vilivyoko kweye tarafa ya Kongwa na kata ya Hogoro .Maeneo yaliopata Mvua zaidi ya mm 600 ni tarafa za Zoissa na Mlali. Katika Ukanda unaopata mvua kodogo mazao makuu yanayolimwa ni Mtama, Uwele, Muhogo na alizeti. Ambapo kanda iliobakia huzalisha zaidi mazao ya mahindi, alizeti na karanga.
KILIMO CHA UMWAGILIAJI:
Wilaya ya Kongwa inaeneo zuri la ardhi linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Mazao yanayofaa na kulimwa katika maeneo haya Oevu ni Mbogamboga na nafaka. Hadfi sasa Wilaya ina skimu zipatazo (4) Mseta Bondeni Tubugwe juu Chamkoroma na Banyibanyi katika kata ya Hogoro. Mazao ya mbogamboga kama Kabich,i nyanya, Vitunguu , pilipili hoho , Mbuzi na viungo vingine yanapatikana kwa wingi katika skimu hizo.
ZANA ZA KILIMO:
Wilaya ya Kongwa ni kati ya Wilaya zenye Matrekta Mengi na hivyo kuleta Ufanisi Mkubwa katika Shughuli za kilimo .Kwa mwaka 2015 Idadi ya Mtrekta ni 731 na Mtrekta ya Mkono ni 43.pia kuna wanyamakazi na zana zao ni 5,032. Kwa mgawanyo auafutao Mksai 3476, Pundas 1556. Kwa sababu ya matumizi makubwa ya Matrekta, Makampuni makubwa matatu yameamua kuweka vituo vya mauzo ya Matrekta na vipuri Kongwa katika Mji wa KIBAIGWA. Makampuni hayo ni pamoja na AGRICOM, SWARAJI- VIPURI na MAHINDRA. Hali hii inawezesha upatikanaji wa zana bora na vipuri kwa maendeleo ya Kilimo katika Wilaya.
VYAMA VYA USHIRIKA:
Wilaya ya Kongwa ina Vyama vya Ushirika vilivyosajiliwa 37 ambavyo vimegawanyika katika Michepuo (7) kama ifuatavyo:
Orodha ya Vyama vya Ushirika Wilaya ya Kongwa:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.