DC KONGWA AKAGUA MIRADI YA ELIMU KATA YA LENJULU
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari – Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka amekagua miradi ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu 6 ya vyoo wenye thamani ya Tsh milioni 64.6 uliopo katika shule ya Msingi Lobilo, ujenzi wa mradi huo unaofadhiliwa na BOOST ulianza Agosti 2025 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 2025.
Baadhi ya miundombinu ya vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Lobilo.
Katika hatua nyingine Mhe. Mayeka amekagua ujenzi wa shule mpya ya msingi na awali mkondo mmoja wenye madarasa 8 na matundu 12 ya vyoo wenye thamani ya Tsh Milioni 302 katika shule ya Sekondari Lenjulu, Mradi unafadhiliwa na BOOST umeanza Septemba 2025 ambapo Mhe. Mayeka amewataka mafundi kuharakisha ujenzi wa miradi hiyo yote ili wanafunzi waanze kuitumia mapema.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.