DED KONGWA AZINDUA DARASA JANJA
Na Bernadetha mwakilabi
Habari – Kongwa DC
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amezindua darasa janja katika shule ya wasichana Kibaigwa litakalowasaidia wanafunzi kusoma Kiteknolojia zaidi.
Baadhi ya miundombinu iliyofungwa katika darasa janja.
Akiongea wakati akizindua darasa hilo Dkt. Nkullo amesema kuwa anategemea mabadiliko makubwa ya kitaaluma katika shule hiyo tofauti na shule zingine Wilayani Kongwa kwani hakuna kisingizio kwa walimu na wanafunzi cha kushindwa kujifunza kutokana na miundombinu ya kisasa iliyowekwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkulo akivishwa skafu na wanafunzi alipowasili shuleni hapo.
Aidha Dkt. Nkullo licha ya kusisitiza kutunzwa na kulindwa kwa muundombinu huo kwa kuweka kamera za ulinzi lakini pia ameshauri wataalamu wa tehema kuweka program ya Akili Unde ili kusaidia kupata majibu ya maswali yanayowatatiza wanafunzi katika ujifunzaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Nkullo akiongea wakati wa akizindua darasa janja.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kongwa Mwl. Sudy Abdul amesema kuwa darasa janja hilo lenye smart board lililofadhiliwa na SEQUIP ni la kwanza katika Wilaya ya Kongwa likifuatiwa na darasa la shule ya Sekongari Manungu.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kongwa Mwl. Sudy Abdul akiongea wakati wa uzinduzi.
Vilevile Mwl. Sudy ameongeza kuwa uwepo wa darasa hilo lenye Televisheni za kujifunzia zilizounganishwa na mfumo wa Intaneti utafanya shule ya wasichana Kibaigwa kuwa bora na kisasa zaidi ambapo mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wa shule nne kwa wakati mmoja na wanafunzi hao wakaonana na kushirikiana kupitia Televisheni hizo.
Akitoa shukrani zake mwalimu mkuu wa shule ya wasichana Kibaigwa Mwl. Gemma Kihwelo ameahidi kuutunza muundombinu huo na kuwasimamia vema walimu na wanafunzi wake kuhakikisha wanajifunza kupata matokeo bora zaidi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Kibaigwa Mwl. Gemma kihwelo akitoa neno la shukrani.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.