TRA KONGWA WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
Na Bernadetha mwakilabi
Habari – Kongwa DC
Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Wilaya ya Kongwa imeadhimisha wiki ya huduma bora kwa mlipa kodi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Wilaya ya Kongwa Bi. Sophia Boma wakati akiongea katika maadhimisho hayo Ofisini kwake mwishoni mwa juma lililopita amesema wanatakiwa kuwa na huduma bora ili wananchi walipe kodi kwa hiari kwani huduma bora kwa mlipa kodi ndiyo nguzo ya Maendeleo.
Bi. Boma ametumia nafasi hiyo kuwashukuru walipa kodi wote wa Wilaya ya Kongwa wakiwemo Wafanyabiashara, Wafanyakazi na Wananchi wote kwa ujumla kwa kusema kuwa ofisi inatambua mchango wao mkubwa wa kulipa kodi.
Meneja Mapato Wilaya ya Kongwa Bi. Sophia Boma akiongea ofisini kwake.
Aidha Bi. Boma amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji kazi, amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka kwa mashauri mazuri ya usimamizi wa kodi, amemshukuru meneja wa mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Dodoma na Kamishna Mkuu kwa usimamizi madhubuti na uongozi imara.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka akilishwa keki na meneja TRA Kongwa.
Nae Bw. Hosea Machako Mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi Kata ya Kongwa amepongeza Ofisi ya Mapato Wilaya ya Kongwa kwa kuwaweka karibu kuwafanya rafiki na kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa hiari.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.