RC SENYAMULE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI KONGWA
Na Bernadetha Mwakilabi
Kongwa - DC
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefanya ziara katika Wilaya ya Kongwa na kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa vyumba 2 vya madarasa ya Elimu ya Awali na matundu 6 ya vyoo katika Shule ya Msingi Kongwa.
Baada ya kusomewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo Mh. Senyamule amemtaka fundi anayejenga majengo hayo kuhakikisha kazi haisimami wala kukwamishwa kwani majengo hayo yanatakiwa kukabidhiwa kwa wakati ili wanafunzi waanze kuyatumia kwa wakati uliopangwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipokea taarifa ya ujenzi katika shule ya msingi kongwa.
Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule amekagua ujenzi wa kituo kipya cha Afya Laikala ambapo hadi kukamilika kwake kitagharimu fedha Tsh milioni 250 na kitahudumia wananchi 28,536 kutoka vijiji 6 vinavyounda kata ya Sagara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Laikala.
Akiongea mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka ameeleza kuwa ujenzi wa mradi wa kituo hicho utafikisha idadi ya vituo vya Afya 10 katika Wilaya ya Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S Mayeka akiongea mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Aidha, Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano mpaka ujenzi utakapokamilika na kuwakumbusha kuhusu zoezi muhimu la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kuwa siku ya tarehe 29 Oktoba wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.