JAMII IMETAKIWA KUTAMBUA HAKI ZA MNYAMAKAZI PUNDA
Na Bernadetha Mwakilabi
Habari - Kongwa DC
Wajumbe wa jukwaa la kumtetea Mnyamakazi Punda Wilaya ya Kongwa wamekutana ili kuunda jukwaa lenye tija juu ya kulinda kwa kufanya ushawishi na utetezi wa mnyama huyo.
Moja ya mjumbe wa jukwaa la kutetea mnyama Punda akichangia mada.
wakichaAkiongea wakati wa kikao hicho mjumbe wa bodi ya Inades Formation Tanzania ambaye pia ni mwezeshaji wa kikao hicho Bw. Patrick Lameck amesema kuwa jukwaa linatakiwa kutambua umuhimu na majukumu ya Punda, kuunda mpango kazi na kujua changamoto wanazozipitia Wanyamakazi punda na kuzishughulikia.\
Mwezeshaji wa kikao Bw. Patrick Lameck akitoa elimu katika kikao hicho.
Aidha Bw. Lameck ameongeza kuwa linatakiwa kuwatambua wadau wengine kama wafugaji, kuunda ushawishi wa utetezi, kutoa elimu na kubainisha shughuli za kufanya na kutoa mrejesho kwa viongozi.
Kwa upande wake mfugaji kutoka Kijiji cha Makole Kata ya Chamkoroma Ndg. Greyson Kusimla amesema kuwa mtetezi wa kwanza wa punda ni mmiliki mwenyewe na kwamba kwa sasa punda amekuwa mnyama wa muhimu amepunguza migogoro ya kiuchumi katika familia kwa kuwasaidia kubeba mizigo.
Ndg. Greyson Kusimla mfugaji kutoka kijiji cha Makole akichangia mada.
Jukwaa limebainisha changamoto zinazowakabili punda kuwa ni pamoja na kuwepo kwa magonjwa na wadudu wanaoathiri ustawi wa Punda, kutokuwa na sheria ndogo zinazowalinda, kubebeshwa mizigo isiyoendana na uzito wao na uelewa mdogo wa jamii kuhusu haki za mnyamakazi punda.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.