KITUO CHA AFYA KUJENGWA KATA YA SAGARA
Mkuu wa Wialaya ya Kongwa Mh. Mayeka S Mayeka amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Sagara kilichopo Kijiji cha Laikala na kuongea na Wananchi wa Kijiji cha Ijaka.
Katika ukaguzi huo mh. Mayeka ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho na ameomba ujenzi ufanyike kwa haraka na kwa wakati ili wanachi waendelee kuona juhudi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Mayeka S Mayeka akikagua kitabu cha vifaa katika ujenzi huo.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho Mganga mfawidhi wa kituo hicho Bi. Maritha Lucas amesema kuwa kiasi cha shilingi Milioni 250 kimeidhinishwa kutoka Serikali kuu kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Bi. Meritha Lucas akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya.
Katika hatua nyingine Mhe. Mayeka ametumia ziara hiyo kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ijaka kilichopo ndani ya Kata ya Sagara kujua kero zao, kuwakumbusha juu ya utunzaji wa mazingira na ulinzi wa vifaa vya serikali na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Ijaka wakiwa katika mkutano.
Akijibu changamoto ya maji inayokabili Kijiji hicho Meneja wa wakala wa Mji Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kongwa mhandisi France Malya amesema kuwa tayari kuna ujenzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 417 wenye tanki la lita laki moja ambao upo katika hatua za mwishoni kukamilika na muda wowote huduma ya maji safi na salama itaanza kupatikana.
Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kongwa Mhandisi France Malya akitoa taarifa katika mkutano huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.