Tuesday 21st, January 2025
@Kongwa - Ukmbi wa VETA
Uongozi wa Wilaya ya Kongwa unatarajia kufanya Kongamano kubwa la maendeleo ya Wilaya siku ya Ijumaa tarehe 17 Septemba, 2021 katika Ukumbi wa Chuo cha VETA Kongwa.
Viongozi mbalimbali wa Wilaya - Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Waheshimiwa Madiwani wa Kongwa, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi za Umma zilizopo Kongwa, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji pamoja na wageni toka Wilaya ya jirani walioarikwa watakuwepo. Kabla, ya Kongamano hili, siku ya Alhamisi kutakuwa na maonesho ya bidhaa na shughuli mbalimbali za vikundi na wajasiriamali wa ndani ya Wilaya ya Kongwa.
Mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Y. Ndugai.
Kauli mbiu ya Kongamano ni “Kutoa huduma bora kwa wananchi ili kufikia maendeleo endelevu ni jukumu letu sote; Tuwajibike kuinua uchumi wa wananchi”
Wadau wote wa maendeleo ya Wilaya ya Kongwa mnakaribishwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.