Sunday 22nd, December 2024
@Uwanja wa Mpira wa Miguu Mkoka
Wilaya ya Kongwa kukamilisha wiki ya Usafi wa Mazingira Duniani leo tarehe 5 Juni, 2018 katika Uwanja wa Mpira wa Miguu Mkoka- Tarafa ya Zoissa.
Katika kilele cha siku hii shughuli mbalimbali zitafanyika ambazo ni; kufanya usafi wa mazingira eneo la njia panda ya NARCO kuelekea Kiteto; Uwasilishaji wa Kaulimbiu ya Usafi wa Mazingira Duniani na Kitaifa; Ujumbe wa Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi; Michezo mbalimbali katika Uwanja wa Mpira wa Miguu Mkoka; na Utoaji wa zawadi kwa washindi wa usafi wa mazingira na washindi wa michezo.
Kaulimbiu ya Wiki ya Mazingira
Kimataifa "Pambana na Uchafuzi wa Mazingira Utokanao na Taka za Plastiki"
Kitaifa na Kiwilaya "Mkaa ni Gharama; Tumia Nishati Mabadala"
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.