Tuesday 21st, January 2025
@St. PIO - Kibaigwa
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Wilaya (Mkuu wa Wilaya) ya Kongwa ameitisha Mkutano Maalum wa Baraza utakaofanyika tarehe 08/09/2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari St. PIO.
Mkutano huu unalengo la kuhamasisha kilimo cha Korosho na Mtama ambacho tunaamini kwa kuendelezwa vizuri kitakuwa na mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa mwananchi na Wilaya kwa ujumla.
Aidha, Mkutano huu utahudhuriwa na wajumbe wa Bodi ya Korosho Taifa na pia, wataalam kutoka Kituo cha Utafiti wa Korosho cha Naliendele.
Hivyo, Wajumbe wa Baraza la Biashara mnaalikwa kuhudhuria Mkutano huu - Wajumbe toka Sekta binafsi, kila mmoja aambatane na wakulima watano wajuu na wakatikutoka katika eneo lake la uwakilishi.
NB:- Washiriki wanaombwa kujigharamia.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.