Saturday 21st, December 2024
@Jimbo la Kongwa - Vituo vya Kuandikisha
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kongwa anawatangazia wananchi wote kuwa Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litafanyika kuanzia tarehe 6 – 12 Desemba 2019.
Zoezi hili linahusisha kuandikishwa Wapiga Kura wapya, kusahihisha taarifa za Wapiga Kura walioandikishwa awali, kuondoa waliokosa sifa, kuhamisha taarifa za Mpiga Kura na kutoa kadi mpya kwa waliopoteza kadi au kadi kuharibika.
Zoezi hili la Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litafanyika katika Vituo vya Kujiandikishia.
Ili uweze kuandikishwa unatakiwa kuwa raia wa Tanzania(kwa Kuzaliwa au kwa Kurithi au kwa Tajnisi) na pia, uwe na umri wa miaka 18 au zaidi au utatimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi 2020.
Kwa msaada kuhusu ufafanuzi wa zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wasiliana na Afisa Uchaguzi 0622750336.
Imetolewa na
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kongwa
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.