Sunday 22nd, December 2024
@Mbande
Kama ilivyo kawaida kwamba Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi huwa ni siku ya usafi Kitaifa. Kwa Wilaya ya Kongwa usafi utafanyika katika maeneo mbalimbali lakini kwa timu za uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Kongwa zitakuwa eneo la Mbande. Aidha, baada ya shughuli za usafi kukamilika, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma atazungumza na wananchi kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu. Wananchi wote wa wilaya ya Kongwa wanaomba kujitoeza katika zoezi la usafi.
Kwa wakati wa zoezi la usafi, maduka yote yafungwa pia shughulizingine tofauti na usafi zisimame kupisha shughuli za usafi atakaye kiuka kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na agizo la Rais.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.