Sunday 22nd, December 2024
@Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Kongwa
Uongozi wa Mradi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara (LIC Project) umechukua washauri toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Biashara kuwasilisha michakato ya njia pendekezwa za urasimishaji wa biashara kushirikisha Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) ya Kongwa na baadhi ya Madiwani wachache.
Uwasilishaji huu unatokana na utafiti uliofanyika mwaka 2016 ambao takwimu zake zilikusanywa na Watendaji wa Kata ambapo walichukua taarifa za ujasiliamali toka kwa wajasiriamali wadogo na wakati walio rasmi na wasio rasmi.
Wajumbe wa CMT wanatakiwa kuhudhuria uwasilishaji huu kwa uwekaji wa maamuzi ya nini kifanyike kulingana na uwasilishaji utakaowasilishwa.
Tukio hili linafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Makao Makuu kuanzia saa tatu asubuhi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.