Sunday 22nd, December 2024
@Hospitali ya Wilaya ya Kongwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ikishirikiana na RITA itafanya kampeni ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto walio chini ya miaka mitano kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 27, Machi, 2019.
Uzinduzi wa Kmapeni hii utafanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, ambapo watoto watakaofika kupata huduma ya kliniki na hawana vyeti watapa fursa ya hii. Vyeti vitakavyotolewa ni bure, mzazi hatagharamia chochote.
Wazazi au walezi wenye watoto ambao wako kwenye umri tajwa hapo juu na hawana vyeti mnaomba kushiriki kikamilifu.
Mzazi au Mlezi anatakiwa kufika na kadi ya kliniki/cheti cha tangazo/cheti cha ubatizo/cheti cha falaki au barua ya uthibitisho wa umri wa mtoto toka kwa mtendaji kata wa kata anayoishi.
Wote mnakaribishwa kwa uzindu huu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.