Sunday 22nd, December 2024
@LAPF Conference Centre
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imesanifu na inaendelea na utengenezaji wa mfumo mpya wa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa wa PlanRep.
Aidha, imetengenezwa mfumo mpya wa Usimamizi wa Fedha za Serikali katika ngazi ya kutolea huduma, mfumo ujulikanao kwa jina la Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS). Mifumo yote hii miwili itazinduliwa kitaifa tarehe 8/09/2017, Kitaifa uzinduzi utafanyika katika Ukumbi wa LAPF Dodoma (LAPF Conference Centre)
Kabla ya uzinduzi kutakuwa na mafunzo ya mifumo yote miwili kwa watumiaji ngazi ya Mikoa na Halmashauri, ambapo mafunzo haya yatatolewa kikanda, kwa Kanda ya Kati mafunzo yataanza Agosti 28 hadi Septemba 8, 2017.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.