Wednesday 15th, January 2025
@Tarafa ya Mlali
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Ndg. Dr. Suleiman Serera anatarajia kufanya ziara katika Tarafa ya Mlali kuanzia tarehe 11 hadi 13 Agosti, 2020. Katika ziara hiyo atasikiliza na kutatua kero za wananchi, atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kujitambulisha rasmi.
Ziara hii itaanza na Kata ya Ngomai tarehe 11/8/2020 saa 3:00 Asubuhi na Kata ya Njoge saa 8:00 Mchana. Tarehe 12/08/2020 atatembelea Kata ya Chiwe saa 3:00 Asubuhi na Kata ya Kibaigwa saa 8:00 Mchana. Tarehe 13/08/2020 atembelea Kata ya Lenjulu saa 3:00 Asubuhi na kumalizia Kata ya Pandambili saa 8:00 Mchana.
Wananchi wote wa tarafa ya Mlali mnakaribishwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.