Tuesday 21st, January 2025
@Shule ya Sekondari Kongwa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison G. Mwakyembe atakuwa na ziara ya kutembelea eneo la Urithi wa Ukombozi lililotumika wakati wa Harakati za Ukombozi lililopo wilayani Kongwa. Aidha, katika ziara hii ataambatana na ugeni wa Waziri wa Sanaa na Utamaduni kutoka Jamhuri ya Afrika Kusini.
Ziara hii ni kutokana na Programu ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Urithi wa Bara la Afrika. Programu ambayo inahusu ukusanyaji, uhifadhi na uwekaji wa kumbukumbu za Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika tangu harakati za kupigania Uhuru wa Nchi za Afrika hadi Bara zima lilipokombolewa mwaka 1994.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.