Kupata Kibali cha Ujenzi Halmashauri ya Wilaya Kongwa:
Kibali cha Ujenzi nikibali kinachotolewa na Halmashauri chini ya Sheria ndogo za Udhibiti wa ujenziholela mijini na ambacho kitamruhusu mwananchi afanye ujenzi au ukarabati wajengo.
Ili kuweza kupata kibali cha ujenzi unatakiwa kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. “Report submitted for Approval (RPA)”. Kuwasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. “Report submitted for Approval (RPA)”. Fomu hii imegawanyika katika sehemu tano (5), zinazohusisha wataalamu wafuatao;
Hatua za Kufuata:
1. Wasilisha michoro iliyokamilika na kujaza fomu inayotolewa na Halmashauri. Fomu itaambatanishwa na michoro iliyokamilika yaani “Architectural & Structural Drawings” na kupita kwa wataalamu wote watano (5) kama ilivyooneshwa hapo juu kwa ajili ya uhakiki.
2. Peleka fomu iliyokamilika kujazwa na viambata vyake kuhakikiwa katika ofisi zifuatazo;
Tanbihi:
3. Mwombaji kuandaliwa kibali cha ujenzikinachosainiwa na mhandisi wa ujenzi na afisa mipango miji.
4. Mwombaji kupatiwa kibali chake tayari kwa ujenzi.
MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI
WAJIBU WA MWANANCHI
Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya mji/jiji kwa kibali kutoka Halmashauri.
TAHADHARI
Kwa maoni na ushauri wasiliana na Ofisi ya Idara ya Ardhi na Maliasili Kongwa: Namba za simu: +255 787 636 917 / +255 762 551 091
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.