FALSAFA
Tunafuata njia ya kijasiriamali katika ushauri wa uongozi wa biashara;
Tunavutiwa kuwa sehemu ya mafanikio ya wateja wetu;
Tunaamini katika ushirikiano na uendelezaji wa mahusiano ya muda mrefu;
Tunahudumia kwa kujitoa kulingana na majukumu yetu.
VIPAOMBELE
UUNGWANA katika kutekeleza na kusimamia matarajio ya wateja wetu;
UAMINIFU kwa kadiri tunavyofahamau hatua sahihi na njia rasmi;
WELEDI WA SOKO tunajiweka kisasa wakati wote kuwa na taarifa muhimu;
UFUATILIAJI kutimiza mahitaji ya mteja;
KUJALI MUDA tunakuita kabla hujatuita;
UFANISI shukrani kwa ujuzi muhimu na mawasiliano katika kutoa huduma za mpango wa biashara wa haraka na unaotekelezeka.
KANUNI NA TARATIBU
1.KUSHINDWA KUTEKELEZA:
Kama hujatoa maelezo ya msingi ndani ya muda, ama hujalipa bili kwa kipindi cha malipo, tuna haki ya kuchukua hatua zaidi za kushughulikia nawe. Na tukishughulika nawe, utalipa gharama za kukufuatilia (faini)
2.MALIPO KATIKA AKAUNTI:
Mara kwa mara unaweza kuhitajika kulipia gharama zote (bili, tozo, faini, kodi, n.k.) katika akaunti sahihi ya Halmashauri katika benki ya NMB. Malipo nje ya akaunti ya Halmashauri, hatutahusika na taratibu za kurejesha katika himaya yako, hivyo zingatia maelekezo na kunakili jina na akaunti za malipo za Halmashauri kwa usahihi.
3.BILI:
Bili zote zinatolewa na mfumo na kwa utaratibu wa sheria na kanuni za Halmashauri ya Kongwa na Serikali Kuu. Kushindwa kulipa ndani ya muda utalazimika kulipa fedha zaidi (faini);
Tuna haki ya kukata fedha zilizoshikiliwa nasi katika akaunti yako, gharama sawa na fedha zisizolipwa kama tozo n.k.
4.HAKI ZAKO:
Wakati wowote, kama una hoja au swali kuhusu kipengele chochote kwa huduma zetu, tafadhali, usisite kuwasiliana nasi.
5.MAELEKEZO YA BAADAYE:
Masharti haya ya utoaji huduma yatahusika kwa huduma zozote zitolewazo na Halmashauri ya Kongwa kuhusiana na tozo mbalimbali, isipokuwa kumekuwa ya pamoja.
“Kituo cha Biashara Kongwa, Tunatoa Matokeo”
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.