Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Mhe. White Zuberi Mwanzalila Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Kongwa, na Katibu wake Bi. Mwanahamis Ally Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, wamepongeza viwango vya utekelezaji miradi katika Halmashauri ya Kongwa.
Pongezi hizo zimetolewa 25 Mei, 2024, na wajumbe wa mkutano wa ALAT utakaofanyika siku ya Jumapili 26 Mei, 2024 Mjini Kongwa. wakati wa ziara ya Ukaguzi wa miradi inayotekelezwa Wilayani Kongwa.
Baadhi ya wajumbe wa ALAT wakiwa ndani ya Jengo la maabara shule ya Sekondari Laikala wakati wa ziara ya Ukaguzi.
Akishauri kuhusu kasi ya mradi wa Jengo la Halmashauri linalojengwa na Mkandarasi SUMA - JKT, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mhe. Donald Mejeti, alishauri mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili kuharakisha ukamilishaji wa jengo hilo lenye ghorofa moja.
Wajumbe wa ALAT wakikagua Jengo jipya la Halmashauri wakati wa ziara ya ukaguzi miradi.
Wakikagua miradi mbalimbali baadhi ya wajumbe wameahidi kupanga muda zaidi wa kufika kujifunza mbinu na mikakati ambayo Halmashauri ya Kongwa imekuwa ikitumia kukamilisha miradi kwa bajeti zilizopangwa, huku sehemu ya fedha ikisalia na kutumiwa kwa ajili ya maboresho miundombinu mingine.
Sehemu ya ndani ya Jengo la Maabara jumuishi (Multipurpose) shule ya Sekondari Laikala iliyojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akipongeza mradi wa Jengo la maabara shule ya Sekondari Laikala, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime aliwataka viongozi kushirikiana na Wananchi kuhakikisha watoto wao wanatumia Miundombinu inayojengwa kujipatia Elimu badala ya kukimbilia mijini kufanya shughuli za ndani.
Diwani wa Kata ya Lenjulu Mhe. Brighton Chisongela ameshukuru ujio wa ALAT Mkoa katika Kata hiyo licha ya Halmashauri kuwa na Kata nyingi, kubwa zaidi akiishukuru Halmashauri ilivyoweza kutoa fedha za mapato ya ndani kujenga Kituo hicho cha Afya ambacho kimeendelea kuboreshwa kwa kujengewa Miundombinu mbalimbali ikiwemo Jengo la maabara.
Diwani Kata ya Lenjulu Mhe. Brighton Chisongela akifurahia jambo pamoja na wajumbe wengine.
Nao baadhi ya Wananchi walipofika Kwenye Kituo hicho cha Afya licha ya kupongeza jitihada za Serikali, pia wameiomba Serikali kuleta wataalamu wa Afya katika Kituo hicho ambacho kwa Sasa kina wataalamu wawili tu, jambo ambalo Mkurugenzi Mtendaji Kongwa Dkt. Omary Nkullo ameahidi kulifanyia kazi kikamilifu.
Miradi iliyokaguliwa na ALAT ni Jengo la Utawala la Halmashauri linalojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, kikundi cha Wanawake cha Ushonaji nguo Kongwa Mjini, Mradi wa Maji Kijiji cha Laikala "B" unaotekelezwa na RUWASA, Maabara jumuishi (Multipurpose ) Shule ya Sekondari Laikala iliyojengwa kwa Mapato ya ndani, na Jengo la maabara ya Kituo cha Afya Lenjulu ambalo pia limejengwa kwa fedha za Makusanyo ya ndani ya Halmashauri.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.