Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Mayeka Simon Mayeka amewataka wananchi wote wa Kongwa kuimarisha amani iliyopo bila kujali itikadi za siasa, dini na ukabila.
Mhe Mayeka ameyasema hayo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo Cha veta Kongwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali na makundi ya wananchi mbalimbali ambapo amesisitiza kuwa amani iliyopo katika nchi ya Tanzania haikutokea tu ila ni kazi ya watangulizi wetu.
"kama tutaacha umoja upendo na amani, maendeleo hayana maana yoyote, miaka 63 ya uhuru tumepata maendeleo makubwa inatupasa tutengeneze mazingira mazuri ya kufikia maendeleo zaidi" amesema Mhe. Mayeka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mstaafu Mhe. Ole Saitabahu ameeleza kuwa Taifa la Tanzania limepiga hatua kubwa sana ya maendeleo na lazima kila mwananchi ajipongeze kwa hatua iliyofikiwa
Ndugu. Saitabahu ameweka wazi kuwa enzi za uongozi wake alitembea kwa miguu wakati akitekeleza majukumu yake sababu hakukuwa na gari la ofisi na pia ameweka wazi kuwa shule nyingi hazikuwa na ubora, akibainisha kuwa hata vyoo havikuwepo ukilinganisha na miaka hii ambapo miundombinu ya kila sekta imeboreshwa na viongozi wote wa Serikali Wana vyombo vya usafiri kurahisisha utendaji kazi wao.
Nae katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa Bi Joyce Mkaugala amefafanua kuwa mada ya Uhuru wa Tanzania Bara inapoongelewa huwa inaambatana na kumbukumbu ya Chama Cha TANU kilichoanzishwa kwaajili ya kupigania uhuru kipindi cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akiongea kwa niaba ya kikundi cha wanawake na Samia Bi. Debora Chambo amesema kuwa miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, nchi ya Tanzania imepiga hatua katika upande wa kupigania haki za wanawake na kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia na watoto.
Sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania bara zimebeba kauli mbiu ya, “UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU.” Kwa dhumuni la kusambaza falsafa ya wananchi kushirikishwa katika hatua za maamuzi ili kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.