Kilio cha siku nyingi kwa wakazi wa wilaya ya Kongwa kuomba barabara ya kutoka Kongwa kwenda Mbande kujengwa kiwango cha lami sasa kimesikika kwani ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umeshaanza.
Kwa sasa mkandarasi ameshaanza kukusanya vifaa na tayari baadhi vimeshafika eneo la mradi. Katika utekelezaji wa mradi huu, jumla kilometa 11 zitajengwa kutoka barabara kuu (Dodoma – Dar es salaam) hadi sehemu ya mizunguko (round about) ya Kongwa. Barabara inatarajiwa kukamilika baada ya miezi tisa (9) kwa mujibu wa mkataba.
Aidha, kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii kutafungua fursa nyingi kwa wakazi wa Kongwa kwani maandalizi ya upimaji wa viwanja kwa maeneo ya Mbande yamekamilika pia ili kuufanya mji huo kuwa wa kisasa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.