Barabara ya NMB - Mlanga imeanza kujengwa kwa kiwango cha lami (double surface dressing) kuanzia NMB kuunganisha kipande cha barabara ya Kilimo-Kwa DAS yenye urefu wa Km 0.88.
Barabara hii inajengwa kwa gharama ya TSh. Milioni 350 na Mkandarasi HEMATEC INVESTMENT LTD wa S.L.P 34078 DAR ES SALAAM, ujenzi unatarajia kukamilika ndani ya miezi nne. Mkandarasi ameanza ameanza kazi tarehe 12/02/2018 na anatarajiwa kukamilika tarehe 11/06/2018.
Lengo kuu la mradi huu ni uboreshaji wa barabara za Mji kwa kiwango cha lami kwa kuunganisha mitaa na maeneo ya jirani.
TARURA ina mkakati wa kupanga bajeti kwa kila mwaka wa fedha ili kuendeleza mtandao wa barabara za lami eneo la Makao Makuu ya Mji Kongwa
Chanzo: Eng. Bwaya S.J (Meneja wa TARURA Kongwa).
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.