Baraza la Biashara la Wilaya ya Kongwa limefanya kikao maalum kuhusu kuweka mazingira bora na rafiki ya kukuza biashara zilizopo pamoja na kuibua biashara mpya wilayani humo.
Mchokoza mada kutoka shirika la uboreshaji wa Mazingira ya Biashara ya Ndani (Local Investment Climate - LIC) Ndugu Donald Liya ameeleza kwamba baada ya Serikali kuhamishia Makao Makuu yake katika Jiji la Dodoma, Mkoa wa Dodoma umekuwa na fursa nyingi za uwekezaji na wadau wengi wamekuwa wakifika katika Ofisi ya LIC Jijini Dodoma kutafuta fursa za uwekezaji. Hivyo, kama Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa haijajiandaa vema itapoteza fursa hii ya Dodoma kuwa Makao makuu ya nchi.
Aidha, amefafanua sehemu zenye mapungufu katika Halmashauri ya Kongwa kuhusiana na masuala ya uendelezaji na uibuaji wa biashara kwa mujibu wa tafiti ndogo iliyofanyiwa na LIC, ambapo amezitaja changamoto hizo ni; huduma kwa wateja (wafanyabiashara au wawekezaji) ikiwemo utoaji wa taarifa sahihi kwa wakati; upatikanaji wa umeme wa uhakika; upatikanaji usioridhisha wa huduma za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali; upatikanaji wa ardhi iliyopimwa kwa ajili ya uwekezaji na biashara; kukosekana kwa taasisi muhimu zinazochochea biashara na uwekezaji kama vyuo, taasisi za fedha (banks), shule nzuri binafsi, kampuni za afya, maeneo ya michezo na burudani, n.k.; utitiri wa tozo kwa biashara – tozo ngazi ya Halmashauri na Serikali Kuu; miundombinu duni hasa kutoka maeneo ya uzalishaji.
Baada ya mchokoza mada kuwasilisha mada, Wajumbe walijadili changamoto zilizobainshwa na kisha kufikia maazimio yafuatayo;
Kikao hiki cha Baraza la Biashara la Wilaya maalum kimefanyika Septemba 12, 2018 ambapo mbali na wajumbe wake limehudhuriwa na wageni walikuwa wakiwemo Wakuu wa Taasisi mbalimbali Wilayani Kongwa, Waheshimiwa Madiwani – Wakuu wa Kamati za Kudumu, na wageni toka Mkoani.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.