Haya yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius John Ndejembi wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Biasharala Wilaya hiyo. Ambapo ameeleza kila alipokuwa akihudhuria vikao mbalimbali kuhusu mabaraa ya biashara nchini Tanzania, Baraza la Kongwa limekuwa likipewa sifa kulingana na jinsi linavyoendesha vikao vyake na utekelezaji wa masuala malimbali ya Baraza. Hii ndiyo sababu ambayo imepelekea hata wafadhi - Mradi wa Uboreshaji Mazingira ya Uwekezaji (LIC) kupeleka miradi mingi katika Wilaya ya Kongwa. Katika Mkutono huu, wamejadili masuala mbalimbali pamoja na kupata elimu kwa mada zilizowasilishwa na wadau wa Ofisi ya TRA.
Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilayani Kongwa wametoa maoni yao juu ya adhma ya kutanua Masoko ya nafaka ikiwemo uanzishwaji wa Soko la Mahindi katika Kata ya Mkoka Wilayani humo mbali na kuwepo kwa Soko la Mahindi la Kimataifa Kibaigwa.
Afisa Kilimo wilaya hiyo Bw. Jackson Shija ambaye ni mjumbe wa Baraza hilo kupitia Sekta ya Umma ametoa maoni yake katika Mkutano wa Baraza Hilo June 27/2018 amesema kutokana na kukua kwa shughuli za kilimo wilayani humo ipo sababu ya kuwa na masoko katika maeneo Tofauti wilayani homo ili kumsaidia mkulima aweze kunufaika na uuzaji wa bei mzuri na Vipimo sahihi.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius John Ndejembi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Kongwa amesema, ana hofu kubwa kuhusiana na kuanzishwa kwa Soko lingine la mahindi na kudai huenda masoko hayo yanaweza kudhoofisha Soko la Mahindi la Kimataifa Kibaigwa.
Aidha, Diwani wa Kata ya Mkoka Mhe. Richard Mwite ambaye alialikwa katika kikao hicho ameeleza kuwa hofu ya kuua Soko la Mahindi Kibaigwa isiwepo kwani wafanyabiashara wengi ambao hununua Mazao moja kwa moja kwa mkulima katika vijiji vya vilivyopo Tarafa ya Zoissa huwa wanasafirisha mazao hayo bila kupitia Soko la Kibaigwa.
"Hivyo uanzishwaji wa Soko hilo kutamsaidia mkulima pamoja na kuisaidia Halmashauri kukusanya mapato katika Soko hilo." Amesisitiza
Kadhalika, Mhe. Ndejembi (Mwenyekiti wa Baraza) amewataka wajumbe wa Baraza hilo, kwa kushirikiana na Madiwani, wataalamu wa Idara ya biashara na Kilimo kujadili kwa kina na kujiridhisha juu ya andiko la mradi huo wa Soko la Mahindi Mkoka kabla ya kupeleka kwa Mradi wa Uimarishaji Mazingira ya Uwekezaji (Local Investment Climate) ambao ndio Wafadhili wanaofadhili miradi mbalimbali inayoibuliwa na Baraza hilo.
Sambamba na hayo amewataka pia, Wajumbe wa Baraza kwa kushirikiana na Idara ya Fedha na Biashara, Kamati ya Mipango na Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa walijadili juu ya punguzo la tozo za karanga zilizobanguliwa kutoka 3000 hadi 1000.
Katika Mkutano huu, wajumbe wamejadili kuhusiana na mradi wa kituo cha mafuta ya alizeti katika kijiji cha Pandambili ambapo eneo la utekelezaji limeshatengwa upande wa kushoto mwa barabara ya kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.
Mradi huo utagharimu milioni 58,018,270/= ambapo Wafadhili LIC watatoa milioni 52,703,270/=, umoja wa wauza mafuta ya alizeti Pandambili (UVIWAPA) watatoa milioni 5,315,000/= na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa itawajibika kuweka umeme na maji katika kituo hicho.
Aidha, utekelezaji wa ujenzi wa awali wa kituo umeanza kama kumwaga mchanga na kokoto kusafisha eneo licha ya kuwa tayari mkataba wa ujenzi huo umeshasainiwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kongwa, Ofisi ya LIC na Umoja wa Vikundi vya wauza mafuta ya alizeti Pandambili(UVIWAPA)
Katika Mkutano huu, Wajumbe wa Baraza wamepata fursa ya kupewa elimu mbalimbali kuhusu masuala ya Kodi ambapo Bw. Barnabas Masika, Afisa Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Ofisi ya TRA Dodoma amewataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari bila usumbufu kwa kutumia mashine za kielektroniki EFD kwani zinasaidia kuondoa usumbufu wa kufuatiliwa mara kwa Mara na watu wa mapato.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.