Waheshimiwa madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wamekaa kikao chao cha mwisho cha kuairisha mkutano Tarehe 19 Juni 2025 kikiwa na ajenda muhimu ya kupitisha sheria ndogo za Halmashauri kutokana na sheria zilizopo kuwa za muda mrefu na kupitwa na wakati.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa kipindi cha miaka mitano mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amesema kuwa katika kipindi hicho Halmashauri imefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo 362 katika sekta zote yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 95 ambazo ni fedha kutoka kwa wananchi, wahisani, Halmashauri na Serikali kuu.
Aidha Dkt Omary Nkullo ametumia mkutano huo kutoa mgawanyo wa walezi wa Kata kwa wakuu wa Divisheni na vitengo ambao watasimamia Kata hizo baada ya baraza la madiwani kuahirishwa.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. Richard Mwite akiongea kwa niaba ya Waheshimiwa madiwani amepongeza na kushukuru ofisi ya mkuu wa Wilaya, mkurugenzi Mtendaji na wataalam kwa ushirikiano na umoja waliouonyesha kwa Waheshimiwa madiwani kwa kipindi cha miaka mitano na kuhakikisha Halmashauri inasonga mbele.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka amesema suala la ulinzi na usalama ni muhimu katika kipindi cha kampeni na amewataka wagombea kujiepusha na masuala ya rushwa katika kipindi cha kampeni na uchaguzi ili kusiwe na dosari katika uchaguzi.
Licha ya kuunga mkono hoja ya utungwaji wa sheria ndogo lakini pia Mhe. Mayeka amekemea vikali tabia ya kuwepo na wizi na upotevu wa Rasilimali katika kipindi cha utekelezaji wa miradi na kuwataka wataalam waliopewa dhamana ya kusimamia Kata kusimamia vizuri Miradi kipindi chote.
Akiongea katika mkutano huo Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa Bi Hella Mlimanazi amefafanua kuwa zoezi la kutunga sheria ndogo ni matakwa ya kisheria kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika Halmashauri zikiwemo kukosekana mpango madhubuti wa usimamizi, uwepo wa mmomonyoko mkubwa wa ardhi mashambani, hasara inayotokana na mafuriko, migogogoro kati ya wakulima na wafugaji na uharibifu wa miundombinu mashambani, Uhaba wa malisho na maeneo ya kuchunga mifugo pamoja na changamoto nyingine.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. Richard Mwite akiongea kwa niaba ya Waheshimiwa madiwani amepongeza na kushukuru ofisi ya mkuu wa Wilaya, mkurugenzi Mtendaji na wataalam kwa ushirikiano na umoja waliouonyesha kwa Waheshimiwa madiwani kwa kipindi cha miaka mitano na kuhakikisha Halmashauri inasonga mbele.
Katika kipindi cha miaka mitano, Halmashauri imefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo 362 katika sekta zote yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 95 ambazo ni fedha kutoka kwa wananchi, wahisani, Halmashauri na Serikali kuu ambapo kila Diwani ameshiriki kufikisha hoja za mahitaji ya Kata yake ili kusudi miradi mbalimbali ya maendeleo ifanyike katika Kata husika.
Ikumbukwe, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka ametoa rai kuhusu suala la ulinzi na usalama na kueleza umuhimu wake katika kipindi cha kampeni na amewataka wagombea kujiepusha na masuala ya rushwa katika kipindi cha kampeni na uchaguzi ili kusiwe na dosari yoyote.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.