Mkutano wa Baraza la Madiwani Kupokea na Kuidhinisha taarifa za Kamati za kudumu ikiwemo Kamati ya Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Maadili, Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, taarifa ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kongwa, taarifa ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kibaigwa kwa kipindi cha robo ya Kwanza (Julai - Septemba, 2024) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umefanyika tarehe 31 Oktoba 2024.
Katika mkutano huo taarifa za taasisi mbalimbali Wilaya ya Kongwa ikiwemo taarifa ya utekelezaji RUWASA, taarifa ya utekelezaji TFS, taarifa ya utekelezaji TARURA, taarifa ya utekelezaji TANESCO, Pamoja na taarifa ya utekelezaji DUWASA pia ziliwasilishwa.
Baadhi ya hoja ambazo zilitolewa ufafanuzi ni Pamoja na mnada mpya wa Visumi ambapo Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na Diwani wa Kata ya Kongwa Mhe White Zuberi amefafanua kuwa mnada mpya wa Visumi utaendelea kusimamiwa vizuri na pia utawekwa pakilio la ng'ombe ili wafanyabishara waweze kununua na kusafirisha ng'ombe zao siku hiyo hiyo na kuwataka wafanyabishara wahamasishwe kujitokeza kwa wingi kufanya biashara katika mnada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Mayeka Simon Mayeka akijibu swali lililoulizwa na Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kongwa kuhusu fidia ya maeneo ya Wananchi yaliyochukuliwa na Jeshi la Wananchi, amesema kuwa suala la fidia ya maeneo ya wananchi yaliyochukuliwa na Jeshi la wananchi wa Watanzania (JWTZ) yaliyopo katika Kitongoji cha Chimlata Kata ya Kongwa tayari linafanyiwa kazi na siku si nyingi Wananchi hao watalipwa fedha zao. Mh Mayeka pia amesisistiza kuwa maeneo hayo yaliyochukuliwa na Jeshi yapo katika mpango wa ulinzi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania hivyo wananchi hawatakiwi kuendeleza shughuli zozote katika maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka akizungumza katika Baraza la Madiwani.
Aidha baada ya kumpongeza mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na timu ya afya kwa kufanya jitihada za ziada kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu, Mh Mayeka amesisitiza kuwa suala la kipindupindu bado linasumbua katika baadhi ya maeneo hivyo amewataka Madiwani kusaidiana na idara ya afya kutoa elimu ya kipindupindu na utupaji taka ngumu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mh Mayeka amewataka Viongozi hususani madiwani kuzuia mihemuko na viashiria vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani katika jamii na ndani ya Nchi ili tuweze kudumisha Demokrasia tuliyonayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa dkt. Omary Nkullo Pamoja na Menejimenti kupitia Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi na walimu wote kwa ujumla wa Wilaya ya Kongwa wamepokea pongezi nyingi kwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa darasa la saba kwani kwa jitihada zao zimepelekea Wilaya ya Kongwa kuwa moja ya Wilaya vinara kwa ufaulu mzuri.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.