Benki Kuu ya Tanzania imeanza kutoa mafunzo ya utambuzi wa noti bandia kwa watu wote Wilayani Kongwa ili kuepuka kupokea au kufanya matumizi kwa kutumia noti Bandia. Mafunzo haya yametolewa na maafisa toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambapo wajumbe waliohudhuria kikao cha maandalizi ya “Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017” Wilayani Kongwa. Katika Semina hii fupi, mada hizi zimewasilishwa; Huduma za Kibenki (kuagiza, kutoza na kutunza sarafu na noti); Kutambua Alama za Noti - ili kuzuia kusambaa kwa noti bandia; na Elimu Kuhusu Hundi.
KUHUSU UTAMBUZI WA NOTI BANDIA:
Wataalam wametoa ufafanuzi kuhusu alama mbalimbali ambazo mtu anaweza kutumia katika kutambua fedha halali kwa matumizi na fedha bandia katika noti za shilingi; 500; 1,000; 2,000; 5,000 na 10,000. Zipo njia tatu za kuweza kutambua noti kuwa ni halali au bandia, ambazo ni;
Njia ya Kwanza: Kuona kwa Macho:-
Njia ya Pili: Kupapasa:-
Njia ya Tatu: kutumia Kifaa Maalum:-
Tumia taa yenye mwanga maalum kuweza kutambua alama ambazo zinaakisi ukizimulika, Kama ifuatavyo;
KUHUSU FEDHA ZILIZOCHAKAA:
KUHUSU UTUNZAJI WA NOTI:
Maafisa wa BoT wasema kwamba fedha zote ni muhimu kutunzwa kwani zinatengenezwa kwa gharama kubwa, hivyo kuharibu ni kulitia hasara taifa. Hivyo, BoT inawataka wananchi wote kutunza fedha za noti kwenye “wallets” au “pochi” kwa akina mama. Aidha, Afisa wa BoT anasema kuwa kuchakaza fedha (note au sarafu) ni kosa kisheria.
Waliopata mafunza haya watakiwa kutoa mafunzo kwa wengine, aidha maafisa hao watakuwa wkitembea maeneo mbalimbali kutoa mafunzo kuhusu utambuzi wa noti kwa wananchi wote, na kuwataka wafanyabishara wakubwa na taasisi zinazopokea fedha nyingi kuwa makini na kuzingatia alama za utambuzi.
Taarifa na Nkinde Moses (Afisa TEHAMA Wilaya ya Kongwa)
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.